Mteja wa Mtambo wa umeme wa Jua kutoka kampuni ya Mobisol Sophia Simon akizungumzia ubora wa vifaa vinavyouzwa na kampuni hiyo na kuwataka watanzania watumie umeme wa nishati ya jua.
Meneja Mauzo wa Mobisol Kanda ya Pwani Wesley Muyenze akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio na mikakati ya kampuni yao katika kuongeza wateja wapya ambapo kwa sasa wana wateja 100,000.
Wateja wakiendelea kupata huduma kutoka kwa watoa huduma wa Mobisol



Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya usambazaji wa huduma za vifaa vinavyotumia umeme unaotokana na nishati ya jua (Mobisol), wamesema kuwa nchi haiwezi kufikia uchumi wa kati wa viwanda bila Kuwa na umeme wa uhakika katika maeneo mengi ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mauzo wa Mobisol Kanda ya Pwani, Wesley Muyenze wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafaniko na mikakati ya kampuni hiyo na kuongezea wateja wanaotumia nishati ya jua ambapo kwa sasa wana wateja 100,000.

Muyenze amesema kuwa kwa sasa watanzania wengi wanauelewa juu ya matumizi ya umeme wa solar hali iliyochangia kampuni hiyo kupata wateja zaidi 100,000 na kuwahudumia watu 500,000.

Alisema umeme wa jua ni chanzo mbadala cha nishati majumbani , pia nishati hii inaweza kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya Viwanda na nchi nyingi tayari zimeachana na vyanzo vya kuzalisha nishati ya umeme vilivyozoeleka kama makaa ya mawe.

Alisema,”nchi haiwezi kufikia uchumi wa viwanda bila Kuwa na umeme wa uhakika katika maeneo mengi ya nchi hivyo kama kampuni watahakikisha wanawafikia wananchi hasa waliopo vijijini ili waweze kuwa na uwezo wa kuzalisha malighafi,”

Muyenze alisema, anawashukuru watanzania ambao wanaotumia nishati ya jua kutoka kampuni ya Mobisol na wapo baadhi yao wameachana na nishati ya umeme inayotokana na vyanzo vilivyozoeleka.

"Hata hivyo kutokana na kuongezeka kwa wateja katika kampuni yetu, tumeamua kutoa zawadi ambapo mteja akinunua mtambo wa W 40 anapata betri na paneli bure kabisa, kwahiyo niwaombe watanzania na wateja wetu wafike madukani kwetu ili waweze kununua bidhaa zetu na kujipatia zawadi hizo, " alisema. 

Aidha alisema anatambua kuwa kuwahudumia wateja zaidi ya 500,000 si kazi ndogo na kuongeza kuwa hali hiyo imetokana na kukua kwa uelewa wa wananchi juu ya matumizi hayo ya nishati ya umeme unatokana na jua. 

Naye Mteja wa mitambo ya umeme inayouzwa katika kampuni hiyo kutoka Tarime, Sophia Simon alisema mitambo inayouzwa na kampuni hiyo ni imara na tangu ainunue haijawai kuzima hata kama mvua inanyeshe wiki nzima. 

Sophia amesema, bidhaa za Mobisol ni nzuri sana na za uhakika ila ametoa ombi kwa kampuni hiyo kupunguza gharama ili kila mwananchi mwenye uhitaji aweze kuipata na kuitumia kwani wapo wengi ila wanashindwa kuwa nazo kutokana na gharama kuwa juu.

Kampuni hiyo pia wamekuwa na utaratibu wa kutoa mtambo wa umeme wa nishati ya jua kwa mkopo wa miaka mitatu utakaomuwezesha mteja kulipa kidogo kidogo ndani ya muda huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: