Harusi sasa imeisha, kila mtu amesharudi kwao. Hakuna muziki tena, hakuna kwaito tena. Harusi yetu ilikuwa nzuri. Nilijitahidi kuandaa harusi ya ndoto yako. Najua ulikuwa ukiangalia sana kipindi cha harusi, ukatamani tuwe na harusi nzuri kuzidi zile zilizokuwa zikioneshwa. Nimejitahidi katika hilo.
Nilichoshindwa ni kuirusha tu 'Live'. Sasa ni historia. Harusi tumemaliza ni muda wa kujenga ndoa yetu. Kilichobaki ni sisi wawili tu. Kila kitu kinachotarajiwa na sisi kinaanza leo.
Maisha yetu hayako kawaida sasa, kuna siku fulani ulikuwa umevaa gauni lako jekundu. Ulionekana mrembo sana siku ile. Ni siku ile ambapo tulienda pamoja kuangalia Sinema pale Mlimani City. Tukiwa tunaangalia sinema nilitamani nikukiss, nilitamanai nikushike kwa jinsi ulivyokua ukinivutia.
Guess what mke wangu...
Sasa nipo na wewe maisha yangu yote, naweza nikakushika muda wowote ninao hitaji pamoja na kukikiss muda wowote ule. Ngoja nikuambie vitu vichache. Sina kitu cha kukuficha kuanzia sasa. Simu yangu unaweza ukaitumia kama yako, unaweza ukaingia IG yangu kama kwako, twitter, JF, na kwingineko.
Mke wangu kuanzia leo mimi nimekuwa mtoto, kwa miaka mitano iliyopita nilikuwa mwanaume mtu mzima. Nilikuwa nikiamka mwenyewe asubuhi, muda mwingine nililala na njaa. Hizi zote zilikuwa changamoto za maisha. Nilirudi gheto kwangu muda wowote niliojisikia. Na sikuwa na mshauri wa karibu mtu wa ku share nae siri zangu. Lakini vyote vimeisha kuanzia sasa.
Nisikie mke wangu Kuanzia leo wewe ni mtu wangu wa karibu kabisa, utakayenikaripia kama nitachelewa kurudi nyumbani bila sababu ya msingi, utakae niamsha asubuhi saa kumi na mbili niwahi kazini, utakae hakikisha silali na njaa. Ninajivunia kuwa na wewe.
Ni matumaini yangu kuwa utakuwa mke mzuri kwangu. Usiwe na hasira sana na mimi nakuahidi nitakuwa mwema kwako. Usinichunguze sana maana huko mbeleni utaanza kujenga taswira ambazo hazipo zikaja kuleta ugomvi kati yetu. Najua muda mwingine nitakusababishia maumivu ya kichwa ila nakuahidi nitakuwa mfumbuzi wa hayo maumivu ya kichwa pia. @aliciousm
Toa Maoni Yako:
0 comments: