Dimo Debwe Mitiki Mwenyekiti wa mbio za Kigamboni International Marathon akionyesho fomu ya kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki katika mbio hizowakati alipokutana na waandishi wa habari katika eneo la michezo la Fun City – Theme and Water Park’ lililopo Kigamboni jijini Dar es salaam leo kutoka kushoto ni mmoja wa waratibu wa mbio hizo Mwani Nyangasa na Meneja wa Fun City Kigamboni Bw. Waqar Haider
Dimo Debwe Mitiki Mwenyekiti wa mbio za Kigamboni International Marathon akifafanua jambo kwa waandishi wa habari alipozungumza nao katika eneo la michezo la Fun City – Theme and Water Park’ lililopo Kigamboni jijini Dar es salaam leo kutoka kushoto ni mmoja wa waratibu wa mbio hizo Mwani Nyangasa na Meneja wa Fun City Kigamboni Bw. Waqar Haider
Dimo Debwe Mitiki Mwenyekiti wa mbio za Kigamboni International Marathon akifafanua zaidi katika mkutano huo.
Mwezeshaji wa Kigamboni International Marathon Bw. Sunir Rodrigues akifafanua mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya mbio hizo.
Waandaaji wa mbio hizo wakiwa wameshika fulana zitakazovaliwa wakati wa mbio hizo mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari leo.

Katika jitihada za kuijengea Jamii uelewa na hamasa juu ya umuhimu wa kutunza afya na Kufanya Mazoezi, Kampuni ya E World (Events World) kwa kushirikiana na wadau mbali mbali inawaletea mbio za Kigamboni International Marathon, mbio hizi zitaambatana na zoezi la Upimaji wa afya katika kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo huazimishwa tarehe 1 mwezi wa 12 kila mwaka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Ndg. Dimo Debwe Mitiki Mwenyekiti wa mbio hizo ambaye pia ni kocha wa michezo ya riadha na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Riadha ya Walemavu Tanzania alisema, Lengo kuu la “Kigamboni International Marathon” ni kuchochea shughuri za kiuchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji,Biashara na vivutio vya kitalii Vilivyopo Kigamboni na maeneo ya karibu, Kuimarisha Afya pia Kuhamasisha michezo ya Riadha kwa maendeleo ya Taifa letu.

Aidha “Kigamboni Marathon” inafanyika kuunga mkono kampeni ya Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha Watanzania kufanya mazoezi ili kuimarisha afya.

Pia Kwa siku za hivi karibuni Tumeshuhudia Viongozi wetu wakihamasisha wafanyabiashara na wadau mbali kuwekeza ndani ya wilaya yetu mpya ya kigamboni, hivyo ni imani yetu kuwa kufanyika kwa „kigamboni International Marathon‟ kutawavutia watu mbali mbali kufika Kigamboni na kujionea uzuri pamoja na fursa zilizopo kigamboni.

Ni ukweli ulio wazi ya kuwa Kigamboni imezunguukwa na maeneo mazuri zaidi ya kimichezo, Utalii na Uwekezaji kuliko sehemu yeyote ile Jijini Dar es saalam na hiyo ni sababu moja wapo inayotupelekea kuamini kuwa „Kigamboni International Marathon‟ ni miongoni mwa mbio bora Tanzania yenye lengo la wakimbiaji wazuri watakao watakaoleta ushindani mkubwa katika Mchezo huu wa riadha Duniani kote.

Kigamboni International Marathon itafanyika tarehe 2 mwezi wa 12, 2018 Katika sehemu yenye mandhari nzuri nay a kipekee kabisa Afrika Mashariki ‘Fun City – Theme and Water Park’ ili kutoa nafasi kwa washiriki kuburudika na michezo mbali mbali ikiwemo kuogelea baada ya mbio. ikiwa na Mbio za urefu wa kilomita 21(Half Marathon), Kilomita 10 na Mbio kwaajili ya watoto, wazee na hata wale wasio na mazoezi ya mara kwa mara (Fun Run) pia zawadi mbali mbali kushindaniwa zikiwemo Medali za dhahabu, Silver na Gold pia Pesa Taslimu kwa washindi.

Kwa niaba ya Kamati ya maandalizi ya „kigamboni International Marathon‟ natanguliza Shukrani kwa wadau wote waliojitokeza kuunga mkono katika Jambo hili lenye tija kwa Maendeleo ya Taifa letu wakiwemo Viongozi wetu ndani na nje ya Kigamboni, wanahabari, Taasisi Mbali mbali, Makampuni na Jamii kwa Ujumla.

Tunakaribisha Ushiriki/ Udhamini wa Makampuni mbali mbali kutoka ndani na nje ya Kigamboni na kunatoa fursa kwa wafanyabiashara waliyopo Kigamboni kuitumia fursa hii kujumuika pamoja na kuonyesha walichonacho lakini pia kufahamiana na kuongeza Marafiki wenye tija.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: