1. Ugonjwa wa Kisukari; hii ni ugonjwa ambao mwili hushindwa kupambana na wingi wa sukari uliopo ndani ya mwili wa binadamu kutoka kwenye chakula anachokula kila siku na hii huweza kusababishwa kutotengenezwa kabisa kwa homoni ya insulin [diabetes type one] au homoni ya insulin kushindwa kuingia ndani ya cell nene[fat cell] ambazo huwepo mtu akiwa mnene sana. Ugonjwa huu unaathiri sana watu wazima kwanzia miaka arobaini kwani wengi wao hushindwa kupambana na uzito.ugonjwa huu unaweza kuanza bila mgonjwa kujua na kuja kujua kama anaumwa katika steji za mwisho ambapo wengi hukatwa miguu baada ya kupata vidonda visivyopona. Hakuna dawa ya kutibu kabisa ugonjwa huu ila kuna dawa za kusaidia kushusha sukari na hutumika kwa maisha  yote.

2. Ugonjwa wa Moyo: mafuta mengi ndani ya mwili wa binadamu hujaa kwenye mishipa ya damu na kuzuia damu kupita kirahisi hivyo moyo hutanuka na kuongezeka ukubwa ili utengeneze presha kubwa ya kusukuma damu ndani ya mishipa hiyo na dakika za mwisho moyo hushindwa kabisa  kufanya kazi. Mgonjwa huyu huhitaji dawa za kuusaidia moyo kufanya kazi kwa maisha yake yote na ikitokea akaacha dawa, moyo unaweza kusimama na kusababisha kifo.

3. Vifo vya ghafla sana: ukichunguza watu wengi ambao wamekufa ghafla ni wenye uzito uliopitiliza na watu hawa hufa usingizini na kukutwa marehemu asubuhi, hii ni kwasababu unene husababisha hali Fulani inaitwa sleep apnoea ambayo muhusika husimama kupumua kwa muda wakati amelala afu anendelea, wakati mwingine kusimama kwa kupumua kunasababisha kifo kabisa.

4. kansa za aina mbalimbali; unene hufanya mwili kushindwa kupambana na seli zinazosababisha kansa hivyo mtu hua kwenye hatari ya kupata kansa ya figo, kansa ya kizazi, kansa ya utumbo mkubwa, kansa ya maini, kansa ya tezi dume, kansa ya kongosho, kansa ya koo, kansa ya matiti, kansa ya mlango wa uzazi na nyingine nyingi.

5. Kuishiwa nguvu za kiume kabisa; kuna kasumba za mtaani wanasema wanaume wembamba wanajua sana kuridhisha wanawake…hii ni kweli kabisa kwani wanaume wanene huchoka sana kwa shughuli ndogondogo na ikifika jioni huwa hawawezi kufanya chochote lakini pia mafuta mengi kwenye mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume hufanya uume  uishiwe nguvu kabisa hivyo matibabu ya nguvu za kiume kwa watu waha ni kupunguza unene tu wala hakuna miujiza yeyote katika hili.

6. Ugumba kwa wanawake; unene husababisha homoni za wanawake kutokua katika mfumo mzuri[unbalanced] na pia wanawake hawa hupata sana kansa za mifuko ya uzazi yaani fibroids hali hii huweza kusababisha kutozaa kabisa. Ni vizuri kama unaona unashindwa kupambana na unene wako uzae mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

7. Magonjwa ya jointi za miguu[osteoarthritis}; mwili hubeba uzito kulingana na urefu wa mtu husika, mtu akiwa mnene sana jointi za mwili hasa za miguuni[knee joints] huanza kuasagana na kusababisha maumivu makali mno na mtu hushindwa kutembea kabisa..hali hii hutibiwa na dawa za maumivu kupunguza makali lakini suluhisho la moja kwa moja la hali hii ni kupunguza uzito.

8. Presha ya damu kama nilivyozungumzia kwenye tatizo la moyo linavyoanza, pia kitu kilekile hutokea kwenye mishipa ya damu mafuta yanapokua mengi... yaani moyo hutumia nguvu nyingi kusukuma damu ili ifikie viungo vingine na hapo ndipo presha ya damu inapoanza. Hakuna dawa ya kutibu kabisa tatizo hili ila kuna dawa watu hupewa kupunguza presha na humezwa maisha yote.

9. Kiharusi [stroke]; hili ni tatizo linalotokea pale ambapo damu inaingia kwa presha kubwa kichwani na kupasua mishipa ya ubongo au mishipa ya ubongo inapoziba na mafuta..hii husababisha upande mmoja wa mwili wa binadamu kupoteza uwezo wake wa kufanya kazi na hii huleta ulemavu wa muda mrefu sana, japokua watu hawa kuna mazoezi wakifanyiwa huweza kurudi kwenye hali zao za kawaida.

10. Matatizo ya kijamii; aina ya maisha ya watu wanene hua tofauti kidogo na watu wengine,  watu wanene hushindwa kujishirikisha kwenye shughuli za michezo, kucheza mziki,kuogelea  na hata kupata ubaguzi wakati mwingine wakati wa kutafuta mpenzi au kazi..utafiti unaonesha asilimia arobaini na moja ya wanaume huacha wanawake zao kwa sababu ya kunenepa na asilimia kumi na nne ya wanawake huacha wanaume zao kwa sababu ya kunenepa.

Mwisho; unene na kitambi sio kuridhika au kawaida ya mtu Fulani HAPANA kwani kuna uwezekano wa kupungua kwa asilimia mia moja kama ukiamua kupunguza unene na kuna uwezekano wa wewe mwembamba kua mnene, kwani vyote hivyo huchangiwa na aina ya maisha tunayoishi yaani ulaji wa chakula na mazoezi.

Mr. Smoothies a.k.a Bravo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: