Na Samuel Nathaniel Sasali.
Kupoteza Uaminifu ni Sawasawa na Kioo Kilichovunjika hakioneshi vizuri.
Siku moja nakumbuka nikiwa na Mkurugenzi wa Mbulu, Manyara Haudson Kamoga @hudsonkamoga Wakati huo tukitangaza wote aliwahi sema Nanukuu "Maisha yetu yangekuwa yanaandikwa kama Kitabu ili kitumike kwa ajili ya wengine kujigunza basi kuna baadhi ya Kurasa tungetamani zisisomwe kabisa, ama zisomwe polepole, ama watu waziruke wasizisome kabisa sababu pengine kurasa hizo nizaonesha sehemu kubwa na maamuzi ya kujinga yaliyopelekea kupoteza kuaminiwa kwetu kwenye familia ama kwenye jamii" mwisho wa kunukuu.
Zipo nyakati unatamani urudishe nyuma uka edit kwanza maujinga ujinga uliyoyafanya ambayo yakapelekea katika gharama kubwa sana kuaminiwa tena. Ni kama siku ambayo uliamua ofisini ki foji saini ya mtu ili upate hela ya mafuta ya gari yako halafu ukakamatwa baadae, ni kama siku ambayo ulikataa kwenda darasani ukatengeneza cheti baadae ukajilaumu, ni kama siku ulikuwa unatimiana picha zako za hovyo na mke wa mtu halafu mumewe akazipata au mume ulikuwa unachat na wanawake wengine halafu mkeo akakukamata au ulikuwa kiongozi halafu ukatumia madaraka yako vibaya au ulifanya ngono zembe ukapata magonjwa au ukapata mimba huo ukurasa kila ukiusoma unatamani urudishe siku nyuma uka edit matendo yako lakini ndo sehemu ya historia ya maisha yako.
Unatamani uaminike tena na Boss wako,unatamani Jamii ikuamini tena unatamani Mkeo ama Mumeo au familia yako wakuamini tena lakini Ukweli ni kwamba kama Kioo kilichovunjika kinavyoonesha taswira isiyo kamili sababu ya nyufanyufa ndivyo ambavyo kuna changamoto kubwa sana kutaka uonekana uko sawa mara moja.
Taswira uliyoijenga kwa miaka mingi inaweza kupotea kwa kitendo cha sekunde 8. Wapo watu ambao wamewahi shindwa labisa rejesha taswira yao sababu damage yake ni kubwa wakapoteza hadhi, wapo watu ambao waliamua kutoa uhai wao sababu gharama ni kubwa sana na wapo watu waliamua kwa namna yoyote ile kulipa gharama ya matokeo ya maamuzi yao.
Usiogope kulipa gharama sababu hakuna jambo litakalodumu milele ukubwa wa uharibifu wa taswira yako ya kwamba Watanionaje?watanichukuliaje?inaweza chukua muda kubwa kumbuka hata hilo nalo litapita na linafaa kuwa funzo la kwenye Kitabu cha Maisha yako.
Yapo mambo yataacha kumbukumbu yenye maumivu, yenye huzuni na isiyovutia kumbuka hiyo ndio maana ikaitwa kumbukumbu. Ili kitu ama jambo liwe kumbukumbu lazima liwe la sasa ama limepita. Na kumbukumbu huwa haiozi.
Yajayo Yanafurahisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments: