Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro akigawa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mablanketi kwa mmoja wa waathiriwa na mafuriko kutoka kijiji cha Mbuguni,ambao walikumbwa na adha ya mafuriko Aprili mwaka huu.
DC Muro akikabidhi msaada wa vifaa vya usafi kwa mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya mbuguni
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro akizungumza na Wakazi wa Mbuguni mara baada ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa waathiriwa wa mafuriko waishio katika kijiji hicho
Baadhi ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro,ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali kama vile mablanketi,vifaa vya kufanyia usafi kwa wanafunzi wa shule, Magodoro na vinginevyo kwa waathiriwa na mafuriko kutoka kijiji cha Mbuguni waliokumbwa na adha hiyo Aprili mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro amefanya ziara kata ya Mbuguni, iliyokumbwa na changamoto ya mafuriko Aprili Mwaka huu, ambapo amewatembelea wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo na kuwafariji kwa kutoka misaada mbalimbali ikiwemo magodoro,mablanketi, vifaa vya kuhifadhia maji dawa za kutibu maji na vyandarua pamoja na vifaa vya chakula kwa kila Kaya 60 zilizoathirika.

DC Muro pia ametoa msaada wa vifaa vya usafi kwa wanafunzi wa Shule ya mbuguni,ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mh.Rais John pombe Magufuli katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata Elimu bora huku akiwa katika mazingira bora ya kusoma.

Wananchi wamemshukuru Mh Rais kwa kumteua Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ambaye tayari ameanza kuwahudumia kwa kuwaletea misaada.

Pia wananchi wamempongeza Rais Magufuli kwa kuendelea kutafuta wadau mbalimbali wa Maendeleo ambao wameanza kuunga mkono jitihada za serikali hususani katika upande wa kukabiliana na majanga kupitia kazi nzuri inayofanywa na Shirika la msalaba mwekundu Tanzania ( Tanzania RedCross )
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: