Klabu ya Soka ya Yanga rasmi imetangaza kujiondoa kwenye ushiriki wa Michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA KAGAME CUP) yaliyopangwa kuanza kutimua vumbi June 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Klabu hiyo, Dismas Ten amesema kuwa barua yakujiondoa imepelekwa TFF na Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, ikielezwa sababu mbali mbali zilizopelekea kujiondoa kwenye mashindano hayo.

Ten amesema Yanga imekuwa na ukaribu wa michezo mingi hivyo kukosa muda wakutosha kwa Wachezaji wake kupumzika.

"Tumecheza Mashindano ya Sportpesa Super Cup nchini Kenya, bado tuna michezo ya Kimataifa, hali hii kwa kweli inaleta ugumu kwa Kikosi chetu ukiangalia kumekuwa na Majeruhi", amesema Dismas

Amesema kuwa Wachezaji wa Kikosi hicho wamepewa mapunziko hadi June 25, ambapo watarejea kwa maandalizi ya michezo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF).

Pia ameeleza kuwa Kikosi hicho kinahitaji muda wakutosha kwa ajili maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: