PICHANI: Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe kwenye kikao na wadau wa Korogwe juu ya hatma ya matumizi ya stendi mbili katika Mji wa Korogwe. Kikao hicho kilifanyika jana Juni mosi, 2018 kwenye Ukumbi wa Halmashsuri ya Mji Korogwe (Picha na Yusuph Mussa).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe mkoani Tanga Hillary Ngonyani akitoa ufafanuzi namna kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Mji Korogwe kilichokaa Mei 25, mwaka huu kiliamua Mji wa Korogwe kuwa na stendi mbili. Ni kwenye kikao cha wadau wa Korogwe juu ya hatma ya matumizi ya stendi mbili katika Mji wa Korogwe, ambacho kiliitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela na kufanyika jana Juni mosi, 2018 kwenye Ukumbi wa Halmashsuri ya Mji Korogwe (Picha na Yusuph Mussa).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji (TD) Korogwe mkoani Tanga Jumanne Shauri akijenga hoja kuwa Mji wa Korogwe kuwa na stendi mbili kutaathiri mapato ya stendi mpya ya Kilole. Ni kwenye kikao cha wadau wa Korogwe juu ya hatma ya matumizi ya stendi mbili katika Mji wa Korogwe, ambacho kiliitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela na kufanyika jana Juni mosi, 2018 kwenye Ukumbi wa Halmashsuri ya Mji Korogwe (Picha na Yusuph Mussa).
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Korogwe Mjini mkoani Tanga Emmanuel Challe akitoa ufafanuzi namna kikao cha Baraza la Madiwani cha Halmashauri ya Mji Korogwe kilichokaa Mei 25, mwaka huu kiliamua Mji wa Korogwe kuwa na stendi mbili. Chama kilibariki stendi mbili. Ni kwenye kikao cha wadau wa Korogwe juu ya hatma ya matumizi ya stendi mbili katika Mji wa Korogwe, ambacho kiliitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela na kufanyika jana Juni mosi, 2018 kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe (Picha na Yusuph Mussa).
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela akizungumza na wananchi kwenye stendi ya zamani ya mabasi Manundu mjini Korogwe. Alifika hapo jana mara baada ya kutoka kwenye kikao cha wadau wa Korogwe cha kujadili matumizi ya stendi mbili katika Mji wa Korogwe, ambacho kiliitishwa na Shigela na kufanyika jana Juni mosi, 2018 kwenye Ukumbi wa Halmashsuri ya Mji Korogwe. Katika mkutano huo na wananchi, Shigela aliwaeleza bayana, stendi itakayotumika kwa mabasi ni ya Kilole. Hiyo ya Manundu itakuwa ya daladala, bajaj na bodaboda. (Picha na Yusuph Mussa).
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela akizungumza na wananchi (hawapo pichani) kwenye stendi mpya ya mabasi Kilole mjini Korogwe. Alifika hapo jana mara baada ya kutoka kwenye kikao cha wadau wa Korogwe cha kujadili matumizi ya stendi mbili katika Mji wa Korogwe, ambacho kiliitishwa na Shigela na kufanyika jana Juni mosi, 2018 kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe. Katika mkutano huo na wananchi, Shigela aliwaeleza bayana, stendi itakayotumika kwa mabasi ni ya Kilole. Manundu itabaki ya daladala, bajaj na bodaboda. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Korogwe Jumanne Shauri, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Korogwe Hillary Ngonyani (wa pili kushoto). (Picha na Yusuph Mussa).

Na Yusuph Mussa, Korogwe

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela ametengua maamuzi ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji Korogwe ya kuruhusu kutumika kwa stendi mbili katika Mji wa Korogwe.

Na badala yake, ameagiza stendi itakayotumika ni ile ya Kilole ambayo Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli aliifungua Agosti 7, 2017, na kuachana na stendi ya zamani ya Manundu.

Aliyasema hayo jana Juni mosi, 2018 kwenye Mkutano uliofanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Korogwe na kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo madiwani, wakata tiketi za mabasi, wafanyabiashara, watumishi na kamati za ulinzi na usalama za wilaya ya Korogwe na mkoa wa Tanga, na kufanya mikutano ya hadhara kwenye stendi hizo.

Pamoja na marufuku hiyo ya stendi ya zamani, pia ameagiza vituo vya maegesho ya magari kwenye barabara kuu ya Dar es Salaam kwenda Arusha kuanzia Mtonga, Mwembeni, Uwanja wa Sokoni, CRDB, Majengo na Kilole viondolewe.

"Kuanzia tarehe ya leo (Juni mosi) stendi ya mabasi itakuwa moja nayo ni Kilole. Na hiyo ni kutokana na kuongeza mapato ya Halmashauri ya Mji Korogwe. Lakini ni lazima turejee kwenye makusudio yetu ya kujenga stendi mpya, nayo ni kukidhi mahitaji ya wananchi kuweza kupata eneo nzuri na la kisasa katika kutoa huduma.

"Uwepo wa stendi ya zamani (Manundu) kufanya kazi, kunaharibu utaratibu tuliojiwekea, kwani badala ya mabasi kuingia Stendi ya Kilole, yanabaki stendi ya zamani, hivyo kuathiri ufanyaji wa shughuli kwenye stendi mpya. Lakini pia stendi zote zilizopo pembeni ya barabara kuu ziondolewe, zinachangia abiria na mabasi kutoingia stendi mpya" alisema Shigela.

Shigela alisema Stendi ya Manundu itumike kama daladala kwa magari yanayotoka kwenye kata za Halmashauri ya Mji Korogwe, bodaboda na bajaj na si vinginevyo, kwani hata idadi ya magari yanayoingia stendi ya zamani iliyoelezwa na madiwani kuwa hayazidi 10, siyo ya kweli, kwani zaidi ya magari makubwa 40 yanaingia stendi ya zamani kwa siku..
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: