Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila ametoa onyo kali kwa wana CCM wanaokiuka kanuni na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuanza kampeni za chini kuwania ubunge na udiwani katika majimbo matatu ya wilaya ya Mufindi akisema wanakwenda kinyume na kanuni za uongozi na maadili.
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Mufindi wakimusikiliza kwa umakini mkubwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila wakati wa ziara yake ya kwanza ya kikazi.
Baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Iringa wakiwa kazini kupata habari kutoka kwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akipokelewa na green gard wa wilaya ya Mufindi na kupewa heshima anayostahili.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila akivishwa skafu nagreen gard wa wilaya ya Mufindi

NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Albert Chalamila ametoa onyo kali kwa wana CCM wanaokiuka kanuni na katiba ya chama cha mapinduzi kwa kuanza kampeni za chini kuwania ubunge na udiwani katika majimbo matatu ya wilaya ya Mufindi akisema wanakwenda kinyume na kanuni za uongozi na maadili.

Akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya wilaya hiyo mjini Mafinga,Chalamila alisema kuwa amesikia kuwa kuna wanachama wameanza kupita pita kuanza kufanya kampeni za chini chini na kusababisha wapunge wa majimbo hayo kutofanya kazi zao kwa ufanisi.

Chalamila aliyataja Majimbo ambayo wananchama hao hao wameanza kupita ni jimbo Mafinga Mji linaloongozwa na Mbunge Cosato Chumi, jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamudu Mgimwa na Mufindi Kusini Meldrad Kigolla.

Alisema kuwa anafanyakazi kwa ukaribu na vyombo ya usalama wa taifa ili kupata taarifa ambazo ni sahihi na kuwabaini baadhi ya wana CCM walioanza kujitengenezea mazingira kwa ajili ya kupata uteuzi katika uchaguzi mkuu ujao kinyume na kanuni hizo za chama.

Chalamila aliwataka viongozi waliochaguliwa na wananchi kufanya kazi kwa kujituma na kukitendea haki chama cha mapinduzi (CCM) ili kiendelee kuaminiwa na wananchi.

Aidha Chalamila alisema katika mazingira ya kusikitisha alisema wana CCM wengine wanaoshiriki kuhatarisha amani ndani ya chama hicho ni wale waliopewa dhamana ya kuwa wajumbe wa vikao vikubwa vya chama na katika onyo lake kwao aliwatahadharisha dhidi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kwao.

“Waacheni wabunge na madiwani waliopo wafanye kazi, wamalize miaka yao mitano kwa uhuru. Mliwachagua wenyewe, wapeni nafasi na kama mnataka kuamua vinginevyo subirini hadi pazia la uchaguzi litakapofunguliwa lakini sio sasa,” alisema Chalamila.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: