Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka Ofisini kwake Juni 07, Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa taarifa fupi ya mkoa kwa Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo(kulia) wakati alipomtembelea ofisini kwakeJuni 07, 2018 Mjini Bariadi na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa Jeshi walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa Nchini wakati alipomtembelea Mkuu wa mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu huyo majeshi Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimtambulisha Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo viongozi mbalimbali wa mkoa huo waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini Bariadi Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi wakati aliomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi Mkoani Simiyu Juni 07, 2018,(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kumaliza mazungumzo na viongozi hao , Juni 07, 2018.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maafisa wa Jeshi walioongozana na Mkuu wa Majeshi hapa Nchini wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka Mjini Bariadi, wakimsikiliza Mkuu huyo majeshi Bariadi alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Simiyu.
Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga, Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakifurahia jambo wakati Mkuu huyo wa Majeshi alipomaliza kuzungumza na viongozi wa Mkoa huo Mjini Bariadi Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Boniventure Mushongi mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi Mkoani Simiyu Juni 07, 2018.
Mkuu wa Majeshi hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiteta jambo baada ya Mkuu huyo wa Majeshi kuzungumza na viongozi Mkoani humo Juni 07, 2018.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.
Jenerali Mabeyo ametoa ushauri huo wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi Juni 07, 2018.
Mabeyo amesema vyombo vya habari vinapaswa kuwahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri na hivyo waondokane na dhana ya kuajiriwa .
“Vijana tunaowachukua JKT ni kwa ajili ya kuwapa elimu na stadi za kazi ili hata kijana akikosa nafasi katika vyombo vya Ulinzi na Usalama anaweza kurudi kijijini akafanya vitu vya maendeleo, mimi nadhani watu wanahamasishana vibaya kuwa kila anayekwenda JKT lazima aajiriwe, ipo haja ya kubadili mtazamo” alisema Jenerali Mabeyo.
“Jeshi linachukua vijana elfu ishirini kwa mafunzo, wanaochukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama hawazidi vijana 2000 sasa hawa wengine 18,000 wanaenda wapi, kama mawazo yatakuwa ni kwenda JKT ili kuajiriwa hatutafanikiwa lakini kama watakwenda JKT kujifunza stadi za kazi kuwasaidia ili ziwasaidie kujiajiri na kubadili maisha yao tutafanikiwa sana” alisisitiza.
Katika hatua nyingine Jenerali Mabeyo ametoa pongezi kwa juhudi zinazofanywa na Mkoa wa Simiyu katika mkakati wa Kilimo cha Umwagiliaji ili kuwa na ziada ya chakula cha kutosha.
“Suala la umwagiliaji halikuwepo katika fikra za watu wengi, walio wengi wanategemea mvua na isiponyesha hawalimi na maisha yanakuwa duni wanaanza kuilalamikia Serikali, lakini sisi hapa tunayo maji ya Ziwa Victoria, Mkuu wa Mkoa nawapongeza sana kwa juhudi zinazofanywa katika kilimo cha Umwagiliaji, zitasaidia kuwatoa wananchi kwenye ufukara” amesema Mabeyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amesema mkoa huo umeweka malengo ya kujitosheleza kwa chakula na kupitia mkakati wa kuwa na mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Mwamanyili wilayani Busega, ambapo amebainisha kuwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo imeahidi kutoa shilingi bilioni 12kwa ajili ya mradi huo.
“Lengo letu kama mkoa ni kuifanya wilaya ya Busega kuwa eneo ambalo linafanya vizuri katika kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa lina maji ya uhakika ya Ziwa Victoria, Benki ya Kilimo wameahidi kutupa shilingi bilioni 12 kwa ajili ya mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji wa Mwamanyil” alisema Mtaka.
Akizungumzia suala la elimu Mtaka amesema mkoa huo umejipanga kiushindani ambapo madarasa ya mitihani. yatakuwa na makambi ya kitaaluma ambazo zitawakutanisha wanafunzi kwa ajili ya kupitia maeneo yaliyo magumu ili waweze kujiandaa vema na mitihani ya Kitaifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: