SEHEMU YA PILI: VIGEZO KUANZISHWA KWA MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA

Na Daniel Sarungi.

Katibu wa Wazalendo, Nasibugani.

Mamlaka za Serikali za Mitaa huanzishwa kwa kuzingatia Ibara 145 na 146 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara hizi zinaelekeza kuanzishwa kwa vyombo vya Serikali za Mitaa katika eneo la Mikoa, Wilaya, Mji na Kijiji.

Ili kutekeleza matakwa haya, Sheria za Serikali za Mitaa zimeweka masharti, misingi na taratibu za kufuatwa katika kuanzisha Mamlaka za Serikali za Mitaa

Vitu vya kuzingatia kuanzisha Wilaya ni pamoja na idadi ya Wakazi, uwezo wa mapato yanayotosheleza kujiendesha yenyewe, pamoja na kuwepo na eneo/ardhi ya kutosha kuwahudumia Wakazi. Bila kusahau lengo kubwa kikatiba ni kuwafikishia Wananchi huduma kwa urahisi hivyo zipo Wilaya zingine zinazoanzishwa kimkakati kulingana na Jiografia ya eneo husika katika kupata huduma.

Kwa sheria hizo hizo ndo ilitengenezwa Wilaya ya Geita yenye takriban watu laki nane, ikiwa ni sawa na wilaya 17 za Pangani. (Wilaya ya Pangani ina takriban watu elfu 46 na bado imepata hati isiyoridhisha kwa Mkaguzi wa hesabu za serikali),

Kwa lugha nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Geita yenye watu laki nane, anaweza kuongoza Mkoa wa KATAVI wenye watu laki tano na akaendelea kupata hati safi

Wakati Wilaya ya Kigoma Ujiji yenye Wakazi takriban laki mbili ikipata hati isiyoridhisha kwa miaka mitatu mfululizo, Wilaya ya Ilemela Mwanza yenye takriban Wakazi laki Tatu na nusu inapata hati safi kwa mwaka wa NNE mfululizo.

Ndani ya mwaka mmoja wa Fedha 2015/16 zilianzishwa Halmashauri Mpya 16 ikiwemo Wilaya ya Kigamboni, Ubungo, Tanganyika, Mpimbwe, Malinyi, Chalinze, Kibiti, Mbinga, Madaba, Songwe n.k

Kwa mujibu wa ripoti mkaguzi wa mahesabu ya Serikali (CAG) 2016/17 Iliyotoka April 2018, iliainisha kwamba ni Halmashauri Tatu pekee zinaweza kujigharamia kwa asilimia mia na zaidi. Halmashauri hizo ni pamoja na
Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, kwa 320% Halmashauri ya Newala kwa 226% Pamoja na Ubungo kwa 100%

Wilaya mpya ya Kigamboni iliyomegwa kutoka Temeke ina uwezo wa kujitegemea kwa 62% ukilinganisha na Temeke ambayo Inajitegemea kwa 31% pekee. Matumizi ya Temeke ni takriban Bilioni 95 huku ikiwa na uwezo wa kukusanya takriban Bilioni 9 pekee.

Halmashauri nyingi ni tegemezi kwa serikali Kuu, zipo Halmashauri ni tegemezi kwa zaidi ya 98% ikiwemo Wilaya ya Butiama

kwa miaka mitatu mfululizo kulikuwa na upungufu wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ikilinganishwa na bajeti iliyoidhinishwa.

Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na Halmashauri ya wilaya ya Siha ndiyo zenye upungufu mkubwa katika makusanyo ya mapato ya ndani sawa na asilimia 68 ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji wa Babati ilikusanya mapato pungufu kwa asilimia 63

Mhe Rais, hali hii inasababisha halmashauri nyingi nchini kushindwa kutoa 10% ya pato la Ndani kwa ajili ya Vijana na Wakina mama na zipo halmashauri zinazocheza na mahesabu ya kwenye vitabu na kuonyesha kwamba hilo fungu la Vijana na Wakina mama wanalitoa lakini halifiki kwa wahusika alafu wanarudisha kama chanzo kipya cha mapato.

Halmashauri nyingi zimekosa sifa ya kuendelea kuwa Wilaya na zimekuwa mzigo kwa Serikali Kuu.

Naomba pita na Mimi katika sehemu ya tatu nikudadavulie kwa undani zaidi katika Wilaya 100 nilizotembelea nchi nzima

#safishawilaya
#safishamajimbo
#twendepamoja
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: