Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (wa pili kulia) akisalimiana na Rais wa Mastercard, Kusini mwa Jangwa la Sahara, Raghav Prasad (wa pili kushoto) kuashiria kuanzishwa rasmi kwa mfumo mpya wa malipo wa Tigo Pesa- Mastercard QR wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wanashuhudiwa na Mkurugenzi wa Mastercard nchini Tanzania, Anthony Karingi (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Selcom, Sameer Hirji (wa kwanza kulia). Wateja wa Tigo pesa sasa wanaweza kutumia mfumo wa Masterpass QR kulipia bidhaa katika maduka na mawakala zaidi ya 1,000 nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (wa pili kulia) akisalimiana na Rais wa Mastercard, Kusini mwa Jangwa la Sahara, Raghav Prasad (wa pili kushoto) kuashiria kuanzishwa rasmi kwa mfumo mpya wa malipo wa Tigo Pesa- Mastercard QR wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo. Wanashuhudiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Selcom, Sameer Hirji (wa kwanza kulia). Wateja wa Tigo pesa sasa wanaweza kutumia mfumo wa Masterpass QR kulipia bidhaa katika maduka na mawakala zaidi ya 1,000 nchini.
Afisa Mkuu wa Tigo, Huduma za Kifedha kwa Mtandao - Hussein Sayed (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa kampuni ya Selcom - Sameer Hirji (wa pili kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania - Simon Karikari (kati), Rais wa Mastercard, Kusini mwa Jangwa la Sahara - Raghav Prasad (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Mastercard nchini Tanzania - Anthony Karingi (wa kwanza kulia) wakishikana mikono kuashiria uzinduzi wa huduma mpya ya Tigo Pesa – Mastercard QR itakayowezesha wateja wa Tigo Pesa kufanya malipo ya kidigitali kununua bidhaa na huduma mbali mbali kwa haraka, usalama na urahisi zaidi bila matumizi ya pesa taslim.
---
Mastercard na Tigo leo wametangaza kuwa WaTanzania wanaweza kutumia App ya TigoPesa kufanya malipo haraka, kwa usalama na wepesi zaidi kupitia Masterpass QR. Mfumo wa QR (Quick Response) sasa upo wazi na tayari umeanza kutumika na wateja wa Tigo katika maeneo mbali mbali ikiwemo madukani, hotelini na sehemu za biashara nchini kote.
TigoPesa Masterpass QR inaondoa ulazima wa kubeba pesa taslim au kadi ya benki. Kwa hiyo hata ukisahau pochi lako nyumbani, bado unaweza kufanya malipo kupitia Masterpass QR. Mfumo huu unakuhakikishia usalama wa kulipia bidhaa na huduma mbali mbali kwa kuscani nembo ya QR inayopatikana katika kaunta ya malipo dukani ukitumia simu janja (smartphone) au kwa kuingiza tarakimu nane (8) za wakala/muuzaji husika ikiwa unatumia simu ya kawaida.
“Tunajivunia kuwa mtandao wa kwanza wa simu nchini Tanzania kutoa huduma hii kwa wateja wetu. Ubunifu huu unakuja kwa wakati muafaka ambapo tunapanua wigo wa huduma zetu za Tigo Pesa. Ni matazamio yetu kuwa Tigo Pesa itakuwa huduma kamili ya kifedha inayowezesha wateja kufanya miamala ya aina nyingi tofauti. Mamilioni ya Watanzania wanapenda kutumia simu zao za kiganjani kulipia huduma na bidhaa. Masterpass QR itawawezesha kulipia huduma na bidhaa hizi haraka, kwa usalama na wepesi,” alisema Simon Karikari, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Tanzania.
Raghav Prasad, Rais wa Mastercard - Eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara alisema, “Lengo letu ni kuiwezesha Tanzania kuwa eneo lenye nguvu za uchumi wa kidigitali barani Afrika. Kwa kuanzisha mifumo bunifu ya kiteknologia tutapunguza matumizi ya pesa taslim na kujenga mifumo thabiti na salama zaidi ya kufanya malipo. Ushirikiano baina ya Mastercard, Tigo na Selcom ni mageuzi yatakayoashiria karne mpya ya uchumi wa kidigitali nchini Tanzania.”
Kwa muda wa sekunde chache tu, muamala wako wa manunuzi unakamilika. Masterpass QR ni njia ya haraka na rahisi ya kufanya malipo ambayo inakubalika katika maduka na maeneo mbali mbali nchini ikiwemo; vituo vya petroli vya Puma, migahawa ya KFC, Pizza Hut na Choppies, supamarket za Shoppers, Maduka ya dawa ya JD Pharmacy, idadi kubwa ya maduka yaliyopo GSM Mall na maeneo mengine mengi.
Kwa kupakua mfumo mpya zaidi ya Tigo Pesa App, Watanzania wataweza kufanya malipo kwa njia ya Masterpass QR kwa kufuata hatua rahisi zifuatazo;
Fungua App yako ya TigoPesa kisha chagua Pay Merchant Masterpass (Lipa Wakala wa Masterpass).
Tumia App yako ya Tigo Pesa kuscani nembo ya QR iliyopo kwenye kaunta ya kufanyia malipo (au ingiza herufi nane (8) za wakala zilizoainishwa chini ya nembo ya QR).
Ingiza kiasi cha muamala.
Ingiza namba yako ya siri (PIN) kuthibitisha malipo.
Wale wasiokuwa na simu janja/smartphone au wanaotaka kutumia menu ya USSD wanaweza kufanya malipo kwa kufuata hatua hizi sita rahisi:
Piga *150*01#
Chagua 5 – Pay Merchant (Lipa Wakala)
Chagua 2 – Pay Masterpass QR merchant (Lipa Wakala wa Masterpass QR)
Ingiza tarakimu 8 za wakala
Ingiza kiasi cha muamala
Ingiza namba yako ya siri (PIN) kuthibitisha malipo
Ikiwa ni sehemu ya kusherehekea uzinduzi wa Tigo Pesa Masterpass QR nchini Tanzania, Mastercard inamtambulisha mcheza soka maaarufu – Lionel Messi, kama sura ya kampeni hii ya uzinduzi, hii ikiwa ni njia ya kuongeza hamu na ufahamu wa watumiaji na mawakala. Gwiji huyu wa soka raia wa Argentina ndiye balozi wa kimichezo wa Mastercard ulimwenguni.
Toa Maoni Yako:
0 comments: