Spika wa Bunge La Tanzania Job Ndugai akitoa hotuba ya ufunguzi wa maonyesho ya wadau wa madini nchini kwenye viwanja vya bunge leo kabla ya kuwasilishwa kwa bajeti ya wizara ya madini jijini Dodoma
Banda la Kampuni ya Shanta Gold Mining wakiwa wanatoa maelezo jinsi kampuni hiyo inavyofanyakazi leo kwenye viwanja vya bunge picha zote na Mahmoud Ahmad Dodoma
SPIKA Job Ndugai akipatiwa maelezo na mmoja ya wafanyakazi wa kampuni ya ACCACIA Gold mining wakati wa maonyesho ya wadau w sekta ya madini kabla ya kuwasilishwa houtba ya bajeti ya wizara hiyo bungeni jijini Dodoma leo
Banda la watafiti wa madini nchini wakimpatia maelekezo mgeni rasmi spika wa bunge Job Ndugai akiwa na mwenyeji wake Waziri wa madini Anjela Kairuki na katibu mkuu Profesa Simon Msanjila kwenye viwanja vya bunge leo
SEHEMU YA VITO VINAVYOPATIKANA HAPA NCHINI NA MAWE YA AINA MBALI MBALI
Wadau wa sekta hiyo kampuni ya uwekezaji ZEM TANZANIA LIMITED kutoka nchini China ambao wanachimba madini ya dhahabu mkoani Mara nao wameshiriki maonyesho hayo wakitangaza dhana mbali mbali za uchimbaji wa madini
Picha juu na chini ni banda la Kampuni ya SHANTA GOLD MINING wakitoa maelekezo kwa mfanyakazi wa bunge aliyepata kutembelea banda lao jijini Dodoma kwenye viwanja vya bunge kabla ya hotuba ya bajeti
Wadau wakisogelea banda la Shanta Gold kupata kujua shughuli wanazozifanya hapa nchini hususani kwenye mikoa ya Mbeya na Singida
Banda la watafiti wa madini nchini kutoka wizara ya madini wakiwa kwenye maonyesho yao kabla ya kuzinduliwa na mgeni rasmi spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai leo kwenye viwanja vya bunge picha na Mahmoud Ahmad Dodoma.
Sehemu ya wadau wakimsubiri spika wa bunge hayupo picha kuja kuzindua maonyesho hayo ya wadau wa sekta ya madini nchi kwenye viwanja vya bunge jijini dodoma leo picha zote na Mahmoud Ahmad, Dodoma.

Na Mahmoud Ahmad, Dodoma.

Spika wa bunge Job Ndugai ameitaka sekta ya madini hapa nchini kuhakikisha wanayapa thamani madini mbali mbali yanayopatikana hapa nchini kwa kuyachakata kabla hayajaingia sokoni lengo likiwa ni kuongeza pato na thamani.

Ndugai ameitoa Kauli hiyo wakati hotuba yake kwenye maonyesho ya wadau wa sekta ya madini kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma, na kuitaka kuhakuikisha wanaongeza thamani madini kabla ya kuingizwa sokoni ndani na nje ya nchi.

Ndugai Ametanaibaisha kuwa uchenjuaji wa madini uende sambamba na kuyapa thamani madini yetu lengo likiwa ni kuongeza ubora wake utakaosaidia kuboresha madini yetu na kuacha kupeleka madini ghafi nje ya nchi.

Ameitaka wizara hiyo na wadau wake kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za utafutaji,uchimbaji na uongezaji thamani madini nchini ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.

“Hapa mnatakiwa kuangalia suala zima la kuyapa madini yetu thamani na kuhakikisha wachimbaji wadogo wanapata dhana bora na kujua maeneo bora ya uzalishaji wa madini hili litasaidia ukuaji wa sekta hili na kuweza kuchangia mapato ya Taifa”

Awali akimkaribisha spika ndugai Waziri wa Madini Anjela Kairuki amesema kuwa wizara hiyo imejipanga kuhakikisha sekta ya madini inanufaisha taifa na kuongeza kuchangia katika ukuaji wa pato la taifa sanjari na kuongeza nafasi kwa vijana kujiajiri.

Hatua nyingine baada ya kufuguliwa kwa maonyesho hayo kwenye viwanja vya bunge waziri huyo akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo bunge ameliomba bunge kumuidhinishia kiasi cha tsh. Billion 58.908 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka 2018-19.

Aidha amesema kuwa sekta ya madini ni muhimu katika kukuza uchumi na kutoa mchango mkubwa kwa taifa na dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 ambapo mpango wa kuhakikisha sekta inanufaisha nchi hivyo wamejipanga kuimarisha ulinzi na kudhibiti utoroshwaji wa madini.

Nae Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Dustan Kitandula Amesema kuwa sekta hiyo itaendelea kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za utafutaji,uchimbaji na uongezaji thamani madini nchini ili kuongeza mchango wa sekta hiyo katika pato la taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: