NA DOKTA MATHEW (SHEA KWA VIJANA WENGI)
• Ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na bateria aitwae NEISSERIA GONORRHOEAE. Ugonjwa huu hushambulia sehemu nyevu na laini za mwili (mucous membrane) ambazo ni njia zetu za uzazi kwa mwanaume na mwanammke,njia za haja kubwa kwa wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile na kooni bila kusahau macho kwa watoto wanaozaliwa kwa kina mama wenye kisonono na unaweza kusambaa na kumuua mtoto .
• Kisonono kwa mwanaume hupenda sana kushambulia sehemu ya mbele ya njia ya mkojo (anterior urethritis).
• Kwa wanawake hupenda sana kuambulia shingo ya kizazi(endocervicitis) na njia ya mkojo(urethritis)
MAKUNDI YALIYO KWENYE HATARI YA KUPATA KISONONO
• Ni vijana kuanzia miaka 15-25
• Wanaofanya mapenzi ya jinsia moja(mwanaume kwa mwanaume)
• Wanaojiuza/makahaba
• Wenye wapenzi wengi
• Matumizi mabaya au kutokutumia kondomu
• Na kama uishawahi kuumwa kisonono huko nyuma.
DALILI ZA MTU MWENYE KISONONO
KWA MWANAMKE
Wanawake wengi wenye kisonono hawana dalili kwa maana hiyo wanapata madhara makubwa ya kisonono bila ya wao kujua kwamba wanaumwa. Sehemu zinzoshambuiwa sana ni shingo ya kizazi kwa asimia 90 ikifuatiwa na njia ya mkojo kwa asilimia 800. Zingine ni njia ya haja kubwa (mkundu) kwa asilimia 40 na koo asilimia 20. Kama dalili zipo mwanake anaana kuziona kuanzia siku 7-10
Dalili ni kama zifuatazo;-
Kutokwa uchafu sehemu za siri
Maumivu wakati wa kukojoa
Maumivu wakati wa kufanya mapenzi.
Kutokwa na damu isiyo hedhi mfano baada ya tendo la ndoa nk
Mamivu ya tumbo chini ya kitovu
KWA WANAUME
Dalili kwa wanume zinaanza mapema sana,ndani ya saa24-48 mwanauume atakua ameshaona dalili zifuatazo
Maumivu makali wakati wa kukojoa(dalili kuu)
Kutokwa na uchafu uumeni(dalili kuu)
Baada ya muda damu yawez kutoka pia
MADHARA YA KISONONO KWA WANAWAKE
Maambukizi ya mirija ya mayai na mayai(PID)
Usaha/jipu kwenye mrija wa mayai Ugumba/utasa
Kovu kwenye mirija ya mayai na kuziba mirija ya mayai
Mimba kuharibika ovyo
Maumivu ya tumbo upande wa juu kulia(perihepatitis)
Mimba kutunga nje ya mji wa mimba
Nawaomba mtag vijana wengi sana waje wajifunze.
MADHARA YA KISONONO KWA WANAWAKE
Maambukizi ya mirija ya mayai na mayai(PID)
Usaha/jipu kwenye mrija wa mayai
Ugumba/utasa
Kovu kwenye mirija ya mayai
Mimba kuharibika ovyo
Maumivu ya tumbo upande wa juu kulia(perihepatitis)
Mimba kutunga nje ya mji wa mimba
KWA WANAUME
Kovu kwenye njia ya mkojo na kuziba kwa mkojo
Utasa/gumba
Kuvimba mapumbu (orchitis)
Maumivu ya viungo
Ukiachana na hizo madhara maalum za kila jinsia,usipotibu huu ugonjwa utasambaa na kushambulia moyo, macho na kua kipofu, ubongo na KIFO. Pia unakua katika hatari ya kuambukiwa magonjwa mengine hasa HIV.
MARA UONAPO DALLI HIZO HAPO JUU WAHI KITUO CHA AFYA ILI UTIBIWE NA KIZURI NA KWAMBA HUU UGOJWA UNATIBIKA.
NAMNA YA KUJIKINGA NA KISONONO
• Subiri/acha ngono.
• Uwe mwaminifu kwa mpenzi mmoja unaeaminiana naye.
• Tumia kondomu kwa usahihi.
• Wahi matibabu mara tu dalili zinapojitokeza.
• Tumia dawa kwa kufuata malekezo ya daktari/usahihi.
• Tibiwa wewe na wenzi wako wote.
UKITAKA HABAZI ZAIDI JUU YA AFYA, MTEMBELEE DR. MATHEW KATIKA UKURASA WAKE https://www.instagram.com/doktamathew/



Toa Maoni Yako:
0 comments: