Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari (kushoto) akizungumza katika hafla ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo, Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado pamoja na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed.

Kampuni hizi mbili zitashirikiana katika bidhaa na promosheni zitakazoboresha huduma kwa wateja wa sasa na wa siku zijazo. Tigo na Uber nchini Tanzania wanatarajia kutangaza ofa zaidi kabambe zitakazowawezesha wateja kufurahia huduma za Uber jijini Dar es Salaam ambapo huduma za Uber zinapatikana kwa sasa.
Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari(wa pili kushoto) akipeana mikono na Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado(wa pili kulia) mara baada ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo na kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
---
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeingia katika makubaliano ya kipekee na kampuni ya kiteknologia ya Uber. Kuanzia leo, wateja wote wa Tigo watatumia huduma za Uber App bure! Makubaliano haya ya aina yake yatawafaidi watumiaji wa huduma za usafiri za Uber pamoja na madereva waliojiunga na mfumo huo.

“Tigo ni nembo pana ya biashara katika soko la Tanzania na tuna wajibu wa kuzindua njia bora zaidi kwa wateja kujumuika katika maisha yanayowazingira. Makubaliano haya na Uber yanaboresha bidhaa na huduma ambazo wateja wetu wanafurahia katika maisha yao ya kila siku,” Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema.

Naye Alfred Msemo, Mkurugenzi wa Uber alisema, “Tunafurahia makubaliano haya na Tigo yatakayowawezesha watumiaji na madereva wa huduma za Uber waliojisajili na mtandao wa Tigo kutumia huduma ya Uber App bure kwenye simu zao za mkononi bila tozo lolote la gharama za data.

Uber ni mfumo wa simu za kisasa unaowezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kubonyeza kitufe tu! Lengo kuu la Uber ni kuwezesha usafiri salama, wa uhakika na kwa gharama nafuu kwa kila mtu, kila sehemu. Makubaliano haya yatawahamasisha maelfu ya wakaazi wa Dar es Salaam ambao wamejisajili na mtandao wa Tigo kutumia Uber App kwa ajili ya huduma za usafiri jijini Dar es Salaam,’ Msemo alibainisha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: