Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye moja ya mashine zilizopo katika karakana ya uhunzi na uundaji wa vyuma akipata maelezo kutoka kwa wanafunzi ambao wanajifunza kupata ujuzi wa fani hiyo na kuja kulitumikia taifa hili hata kuanzisha viwanda vidogo vidogo au kwenda kufanya kazi kwenye viwanda mbalimbali
Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akipata maelezo kutoka chumba cha kompyuta ambacho nacho kipo chuoni hapo
Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye chumba cha mapishi ambako wanafunzi wa fani ya upishi huwa wanajifunza kwa vitendo.
Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye karakana ya umeme
Hii ni karakana ya useremala ambayo pia inawaongezea ujuzi wanafunzi wa fani hiyo ikiwa na vifaa vya kisasa kabisa
Na Fredy Mgunda, Iringa.
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kupitia chuo cha ufundi VTC Mdabulo kilichopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa linawasaidia watoto yatima na walio kwenye mazingira magunu kwa kuwapatia elimu ya ufundi bure.
Akizungumza na blog Mkurugenzi mtendaji wa R.D.O Fidelis Filipatali alisema kuwa shirika hilo linawasomesha wanafunzi bure wanatoka katika mazingira magumu na watoto yatima ili kuwapa elimu itakayowakomba katika maisha.
“Lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo mengine kwenye vyuo vingine wanapata nafasi katika chuo chetu hiki ambacho kinagharama nafuu na kinatoa elimu bora ya ufundi ambayo inatamsaidia huko mbele kwenye maisha yake” alisema Filipatali
Filipatali alisema kuwa shirika hilo limebeba dhima ya Rural Devolopment Organization (RDO) kwa kutoa ujuzi endelevu kwa jamii ili kuondokana na kuwa tegemezi katika maisha na kuishi kwa kujitegemea kutokana na ujuzi unaopatikana chuoni hapo.
“Chuo cha ufundi stadi cha RDO VTC na shirika kwa ujumla vinanuia kuinua jamii kutoka a hali ya chini kiuchumi na kufikia hali nzuri ya kimaisha na ndio maana tupo huku vijijini ambako ndio kuna wananchi wengi wa hali hiyo” alisema Filipatali
Lakini Filipatali alisema kuwa chuo hicho kimelenga kuwapa ujuzi wa muda mfupi na muda mrefu kwa lengo la kuwasaidia kuendelea kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo.
“Tunatoa ujuzi kwa njia tofauti tofauti hivyo tunapoona kuwa wanafunzi wanauwezo wa kujitegemea na wapo tayari kwenda kujitegemea huwa tunawaruhusu ili kupisha nafasi kwa wanafunzi wengine kupata ujuzi wa kiufundi” alisema Filipatali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: