Jeffrey Jessey anaishi ndoto ambayo kila kijana wakitanzania angependa kuishi hivyo. Akiwa na ari ya kuja kuwa na mafanikio Jeffrey alianza shule hadi kufika Chuo kikuu cha Dar es salam ambako alisoma masomo ya biashara huku akisaidia wanafunzi wenzake kupunguza nguo kubwa na kuzifanya kuwa “modo“.
Jeffrey ambaye maisha yake ya nyuma yalikuwa na changamoto nyingi ambazo zilipelekea kuuza maji ili kuifanya familia ijikimu.
Kwa uhakika mafanikio yake ya leo yanachangiwa sana na makuzi yake yaliyomtayarisha kupambana na kufanikiwa.
Baada ya kumaliza shahada yake ya chuo kikuu, Jeffey hakutaka kuajiriwa bali kujiajiri kama mshonaji wa nguo kupitia chapa yake ya Speshoz. Hadi sasa ameajiri watu wengi na kufanikiwa kutengeneza jezi za Yanga, kuwavesha Diamond Platnumz, Mfanya biashara maarufu Bakhresa, Wabunge , Mawaziri na Maharusi wengi.
Simulizi ya Jeffrey imo kwenye kipindi maalum cha kukuza Ujasiriamali chenye kulenga zaidi vijana kiitwacho Extra Mile Show ambacho kimezinduliwa leo jijini Dar es salaam.
Wakieleza mkakati wao Extra Mile Show walisema vipindi hivi vinavyopatikana kwenye mitandao na youtube, facebook, instagram na twitter kinalenga kuwawezesha vijana kutambua fursa na kubadilishana uzoefu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: