Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akizungumza na watoto yatima wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam alipotembelea kituo hicho hivi karibuni na kutoa misaada mbalimbali. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila na Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa hilo, Leonard Masano wakisaidiana kupanga misaada mbalimbali zikiwemo nguo na vyakula walivyokabidhi kituoni hapo hivi karibuni.
Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi, akimkabidhi Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba moja ya bidhaa zilizowasilishwa hapo kwa ajili ya matumizi ya watoto wa kituo hicho. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa la Ukombozi, Leonard Masano.
Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akigawa zawadi ya juisi kwa mtoto Godfrey Steven anayeishi kituoni hapo wakati wa kukabidhi mahitaji mbalimbali kwa kituo hicho.
Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akiendelea na zoezi la ugawaji zawadi mbalimbali kwa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam.
Watoto wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luisi, Ubungo Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, Esther Pilila katika hafla ya kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyofanyika hivi karibuni kusherehekea mwaka mpya. Misaada hiyo ikiwamo chakula na mahitaji ya shule ilikabidhiwa kwa kituo hicho na kanisa la Ukombozi.
Mtoto Grace Tegete (1.5) anayelelewa kwenye kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam akifurahia ndani ya gari la mmoja wa wanaukombozi waliofika kituoni hapo.
WATOTO wanaolelelewa katika vituo vya kulea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi wametakiwa kujitambua na kujikubali ili kutekeleza wajibu wao wa kupokea malezi mema.
Aidha imeelezwa kuwa watoto wanathaminika sana ndio maana wapo watu wameamua kujitolea kuhakikisha wanaishi maisha ya kawaida na kuwa watu muhimu katika jamii.
Kauli hiyo imetolewa na Mchungaji msaidizi, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, wakati akizungumza na watoto wa wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis hivi karibuni.
akimkabidhi Mama mlezi wa kituo cha yatima cha Watoto Wetu Tanzania kilichopo Mbezi Luis, wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam, Getrude Nyalubamba (kushoto) akiwa ameongozana na Mwenyekiti kamati ya Msamaria mwema ya kanisa la Ukombozi, Leonard Masano (kulia) walipowasili kituoni hapo kwa ajili ya kukabidhi misaada mbalimbali.
Mchungaji huyo na kundi la wanawake na wanaume wa kanisa hilo walifika kituoni hapo kutembelea watoto hao na kuwapa zawadi mbalimbali.
Alisema katika hafla hiyo kwamba watoto hao wanapojiamini, kujikubali na kujithamini wataona manufaa yake hasa kwa kukubali malezi na kutambua uwepo wa walezi ambao wanajali maslahi yao.
Aidha alisema kwamba ni wajibu wa jamii na kanisa kwa ujumla kutekeleza kwa vitendo kujali yatima wajane na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwa kitendo hicho kina Baraka kubwa.
Alisema kwamba amefurahishwa kufika katika kituo hicho na kutekeleza wajibu wa kukaa pamoja na watoto hao na kumpongeza mama mlezi kwa kazi yake kubwa anayoifanya katika kuwahudumia watoto takribani 31 wanaoishi hapo.
Aliwataka watanzania kuwa na tabia ya kujali watoto hao kwa kuhakikisha wanapata mahitaji yao kila siku na sio siku ya sikukuu tu.
Kituo cha Watoto Wetu Tanzania kilihamishwa kutoka Stop Over kwenda Mbezi Luishi ili kupisha matakwa ya sheria ya barabara ya Morogoro.
Naye mmoja wa watoto 130 waliopita katika mikono ya kituo hicho tangu kianzishwe 1998, Oscar Gabone mwanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe aliwataka wananchi kufika kuwatembelea watoto hao na kuzungumza nao kuonesha upendo hata kama hawana kitu cha kuwapeleka.
Alisema kituo hicho kina changamoto nyingi hasa zinazotokana na kubomolewa kwa makazi yao Stop Over na kwamba juhudi za kujenga maboma ya wanawake na wavulana yanaendelea sio kwa kasi inayoridhisha.
Alitaka wananchi kuchangia ustawi wa watoto wa kituo hicho ambao wengi wamefikishwa wakiwa wadogo na wengine wakubwa kwa lengo la kuwapatia elimu na matunzo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: