Wananchi wa Mbezi Kwa msuguli kuelekea Malamba Mawili wameiomba serikali kuweza kuwanusuru na janga la barabara mbovu.

Wakizungumza na Kajunason Blog mara baada ya kunyesha kwa mvua ya leo Jumatatu Januari 8, 2018 wakazi hao wametoa kilio chao kwa serikali kuwanusuru na barabara mbovu ambayo si rafiki katika shughuli zao za kila siku.

Bi. Somoe Mjata ambaye ni mkazi wa Masaki alisema kuwa kwasasa kilanmvua inaponyesha hata nauli za bajaji na pikipiki ambao ndiyo usafiri wao mkubwa zinapanda.
"Ndugu mwandishi kiukweli hali imekuwa mbaya sana hatuna jinsi maana maisha nayo yamekuwa magumu, nauli kutoka Mhezi Kwa Msuguli kuja Masaki nauli kawaida huwa 500/- kwa bajaji ila mvua ikinyesha tu inapanda mara mbili inakuwa 1,000/- na pande wa pikipiki ni 1,000/- ila mvua ikinyesha tu nayo inakuwa 1,500/- kwa maisha haya ya mwananchi wa kawaida tunawezaje?," alisema bi. Mjata.

Nae Mzee Kalisa Kachuchu aliiomba serikali kusaidia huduma hiyo muhimu kwa vile hata wakipata wagonjwa usiku suala la kupata usafiri linakuwa gumu kwa ubovu wa barabara.

"Mimi bibafsi mwenyezi Mungu amenijalia kuwa na gari ila sioni utamu wa gari hili kama ikinyesha mvua siwezi hata kutoka nalo maana barabara si rafiki na mazingira, yani tunamuomba Rais wetu mpendwa Dkt. John Magufuli kusikia kilio chetu maana eneo hili kama limefumbiwa macho japo viongozi wapo wamelala usingizi," alisema Mzee Kachuchu.

Baada ya Michuzi Blog kutembelea maeneo mbali mbali ya Mbezi Kwa Msiguli kuelekea Masaki na Malamba Mawili iliweza kuona changamoto ya barabara ambayo wananchi wamekuwa wakiipigia kelele kwa muda mrefu licha ya viongozi wao kufumbia macho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: