Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Up Cut' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Aman Bariki utakaofanyika Feb 14 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro. Picha na SUPER D BOXING NEWS.
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Up Cut' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Aman Bariki utakaofanyika Feb 14 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro.
Na Mwandisahi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi ameingia kambini kwa ajili ya mpambano wake na Amani Bariki 'Manny Chuga' mpambano wa raund 8 utakaofanyika katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Feb 14 mpambano uho utakwa wa utangulizi kabla ya mpambano mkubwa utakaowakutanisha.
Twaha Kiduku wa Morogoro na Chiota Chimwemwe wa Malawi mpambano wa raundi 10 mpambano uho wa kimataifa utawakutanisha mabondia hawo baada ya kila mmoja kucheza mpambano mmoja na kushinda na kufanikiwa kukutanishwa kwa viwango vyao
Bondia Mbilinyi anaenolewa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amejinasibu kuwa atacheza kufa na kupona kwani njia ya kuelekea mafanikio yake itakuwa ni hiyo kwa kuwa yeye ni bondia mzowefu ivyo Bariki awezi kumsumbua ata kidogo ajiandae na kipigo cha mbwa mwizi siku hiyo si ya mchezo mchezo nitacvheza kufa na kupona alisema Mbilinyi
Nae promota wa mpambano uho Kaike Silaju amesema ameamuwa kuandaa mpambano huo mjini Morogoro baada ya kuombwa na mashabiki wa mkoa wa morogoro nae bila hiyana nikamua kuleta mpambano huu kwa mara ya kwanza wayu washamzoea Fransic Cheka sasa huyu ndio atakae mrithi Cheka kwabi Kiduku ni bondia bora sana mchini Tanzania hivyo mashabiki mjitokeze kwa wingi mje mshudie mpambano wa kufungulia mwaka
Mbali na mchezo wa masumbwi siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali ambapo kutakuwa na wasanii nao wataonyeshana umwamba ambapo Vicent Kigosi 'Ray' atapambana na Jacob Steven 'JB' uzito wa juu hivyo siku hiyo si yakukosa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: