# Nimekusiliza kwa makini Sana toka Jana na nimekua nikiirudia mara kwa mara clip yako ili nipate kujua Ulikua ukimaanisha nini. Katika kipande kile cha sauti nimekusikia ukilalamika kua raisi Magufuli hataki kushauliwa. Naomba nikuulize, Hivi unajua maana ya Ushauri? Naje unajua katiba inasema nini kuhusu Ushauri anao pewa raisi?
# Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Sura ya Tatu ya katiba inayoelezea haki na wajibu wa Raia, ibara ya 37 kifungu kidogo cha Kwanza kinasema na nitanukuu "37. -(1) Mbali na kuzingatia masharti yaliyomo katika Katiba
hii, na sheria za Jamhuri ya Muungano katika utendaji wa kazi na shughuli zake, Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuataushauri atakaopewa na mtu yeyote, isipokuwa tu paleanapotakiwa na Katiba hii au na sheria nyingine yoyote kufanya jambo lolote kulingana na ushauri anaopewa na mtu au mamlaka
yoyote."
# Nafikiri utakua umenielewa nini nilikusudia kusema, Kila mmoja anashauri kwa namna anavyoona yeye inafaa lakini rais anafuata katiba hivyo haruhusiwi wala halazimishwi eti kutembea kazi Ushauri wa mtu. Atafanya hivyo tu pale anapoona inafaa.
# Baba askofu unapaswa ujue maana ya Ushauri, Ushauri maana yake ni Mawazo ama mapendekezo anayo pewa mtu juu ya jambo fulani. Na mapendekezo hayo yaweza kukubaliwa ama kutaliwa, sasa yanapo kataliwa kwanini iwe nongwa?
# Baba askofu ukiisoma biblia vizuri katika kitabu cha injili ya Luka, Yesu alipo kua mlima sayuni akiomba na kulia huku jasho Kama matone ya damu yakitililika mpaka chini akiomba kwa Mungu kua,kama ikimpendeza amuepushie kikombe hiki cha Mateso lakini mapenzi ya Mungu ya timie na sio Ya kwake Yesu.
# Huu Ulikua ni Ushauri wake Yesu kwenda kwa Mungu, na Mungu alipo iona Hofu ndani yake alimtuma Malaika kuja kumtia moyo na yaliyoandikwa yakatimia.
# Hivyo baba askofu Kakobe Ushauri unaotolewa na watu mbali mbali usiufanye kua ati kwamba ni Lazima Raisi autekeleze.
# Hata wewe nakumbuka Ushauri uliopewa wa kuondoa kanisa hapo lilipo ulikataa na mpaka ukawavika T-shirt waumini wako kuiomba Tanesco Umuogope Mungu. Sasa kama wewe ulishindwa kufuata ushauri inakuaje iwe halali kwako kwa wengine iwe dhambi?
# Note Injili ya Luka Yesu anasema,mbona unakitazama kibanzi kilichomo katika jicho la nduguyo ilihali huoni boriti iliyo Katika jicho lako mwenyewe.
# Mnafiki wewe toa boriti katika jicho lako kisha uje utoe Kibanzi kwa nduguyo.
Imeandikwa na Ngariba Mkuu,
Machame, Kilimanjaro- Tanzania.
27/12 /2017
Toa Maoni Yako:
0 comments: