Waandishi wa habari wakijadiliana kwa pamoja na wadau kutoka Asasi za kiraia mapaema jana jijini Dar es salaam.
Miongoni mwa haki muhimu za binadamu ya kwanza ni kuishi na ya pili ni kupokea na kutoa taarifa katika jamii kwa usahihi.
Hayo yamesemwa mapema jana Kunduchi Beach na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sharia na Haki za Binadamu Bi. Anna Henga katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo ambayo iliwakutanisha waandishi wa habari na watu wa asasi za kiraia.
Anna Henga alisema lengo kuu la semina hiyo ni kuwakutanisha wanahabari na wadau mbalimbali kutoka katika asasi za kiraia (Azaki) kujaribu kuwaweka pamoja na kuona kwa jinsi gani wanaweza kufanya kazi pamoja licha ya kuwa wanawekewa sharia ngumu zinazowabana.
Aliendelea kusema kuwa haya makundi mawili yanategemeana kwa kuwa wanahabari wanategemea kupata habari katika azaki na wana azaki wantegemea wanahabari ili kufikisha ujumbe wao kwa jamii husika.
Lakini pia kuunganisha nguvu za pamoja endapo mmoja wao atapata tatizo katika kazi yake basi kundi linguine liweze kutoa ushirikaiano wa kuona wata msaidia vipi mwanaharakati mwenzao, kwani kwa sasa kuna sharia ngumu zinazoyabana makundi yote mawili.
Bw. Fungis Masawe kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu akitoa elimu ya sheria kwa waandishi wa habari pamoja na wana azaki mapema jana Kundichi Beach jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake bw. Fungis Masawe ambae yeye ni mwanasheria anyefanya kazi na kituo hicho alisema kuwa kunasheria ya mitandao ya mwaka 2015 ambayo inalenga wananchi wote endapo watatuma au kupokea taarifa zisizo rami basi sharia itafuata mkondo wake.
Hivyo wananchi wanatakiwa kuwa macho sana ili wasije wakaingia kwenye ujinai kwani mtu atakeyetenda kosa hili atahesabiwa ametenda kosa la jinai, na wananchi wanatakiwa kupewa elimu ya kutosha katika matumizi ya hii mitandao kama facebook, watsaap nk.
Washiriki wa semina ya wanahabari pamoja na wadau kutoka asasi za kiraia iliyoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wakiwa katika picha ya pamoja mapema jana Kunduchi jijini Dar es salaam.
Na pia alisema kuwa sheria hii inambana mtoa taarifa lakini haikutoa muongozo kwamba nini afanye mtu huyu endapo mtu Yule ambaye ni chanzo cha habari akigoma kutoa taarifa wakati mtoa taarifa atakapohitaji kujiridhisha kwa chanzo chake.
Bwana Fungis aliendelea kusema kuwa kuna sheria ya takwimu ambayo nayo inakataza kutoa takwimu hata kama ni za kweli mpaka utakapopewa idhini na idara husika la sivyo unahesabiwa unakosa la jinai kwa kutoa takwimu bila ruhusa hali inayofanya kukosekana kwa ukweli wa vitu vingi katika nchi yetu
Toa Maoni Yako:
0 comments: