Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (katikati) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akikabidhi vifaa, bidhaa na mahitaji mbalimbali ya watoto wa kituo cha Amani cha watoto yatima, kilichopo Bagamoyo kwa Mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Margareth Mwegalawa (kulia) katika hafla fupi iliyofanyika kituoni hapo Bagamoyo. Kushoto ni , Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Ukombozi tawil la Dar es Salaam, Esther Pilila. Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kanisa hilo, watoto pamoja na walezi wa kituo hicho. Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam katika picha ya pamoja na wakinamama wa kanisa hilo na walezi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi msaada huo. Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akigawa chakula kwa watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo mara baada ya kukabidhi vitu mbalimbali kituo hapo. Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akishiriki chakula cha pamoja na watoto yatima wa kituo cha Amani kilichopo Bagamoyo.
WATANZANIA wamekumbushwa kuwajali na kuwangaalia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwatimizia mahitaji yao ya kimwili na kiroho.
Aidha, wamepaswa kutambua kwamba wana wajibu wa kusaidia watoto hao kwa kuwa wanawekeza kwa manufaa ya taifa na wao wenyewe.
Kauli hiyo imetolewa na Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam, akizungumza baada ya kukabidhi vifaa, bidhaa na mahitaji mbalimbali ya watoto yatima wa kituo cha Amani, kilichopo Bagamoyo, kiasi cha kilomita 65 kutoka Dar es salaam. na Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (mwenye gauni la bluu) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akizungumza jambo mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani, Margareth Mwegalawa (katikati) kukabidhi vitu mbalimbali kituoni hapo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa kanisa, waumini na wamama.
Akitoa maneno yanayogusa nyoyo huku akikariri maandiko Mchungaji Faith alisema:“Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu baba ni hii, kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa”
Alifafanua kwamba Kanisa lisiloangalia yatima na wajane si Kanisa, alisema na kuongeza kuwa waumini wanastahili kuwajibika kwa hilo.
Aidha, alisema kama Kanisa wanajali watoto na ndio maana wamefunga safari kwenda kuwaona na wamefurahi kuwaona na kushiriki nao tafrija fupi baada ya kuwakabidhi zawadi mbalimbali. Baadhi ya wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam wakishiriki maombi baada ya kuwasili kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani kilichopo katika kijiji cha Zinga, mjini Bagamoyo.
Alisema kwa kuwezesha utulivu wa watoto hao, watoto watamjua Mungu na hivyo kujenga taifa lenye maisha yenye utukufu wa Mungu.
Naye, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Esther Pilila alisema kwamba kama wanawake katika Kanisa lao wamesukumwa na haja ya kuwaangalia watoto hao kama wajibu wao.
Akizungumza kushukuru Mkurugenzi wa kituo hicho Margareth Mwegalawa aliomba watanzania kuwakumbuka watoto hao na kuitafadhalisha serikali kuwapitia kila mara kwa kuwa wao ndio walezi wa watoto. Pichani juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam walioshiriki tafrija hiyo. Mwana wa Nabii BG Malisa Mchungaji, Faith Tetemeko (mwenye gauni la bluu) wa Kanisa la Ukombozi tawi la Dar es Salaam akicheza sambamba na mtoto Haji Joseph (11) katika tafrija fupi ambapo Kanisa la Ukombozi lilikabidhi vitu mbalimbali zikiwemo sare za shule, vyakula, madaftari, nguo na mahitaji mengine ya kujikimu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: