Mkurugenzi wa halmashauri ya Kilwa Zablon Bugingo kulia akitoamaelezo ya mradi mkubwa wa uoteshaji wa miche ya korosho kwa Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai
Afisa kilimo na ushirika wilaya ya Kilwa John Mkinga kushoto akitoa taarifa ya mradi wa uoteshaji wa miche ya korosho mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda alipofanya ziara leo Wilayani humo.
Picha ikionyesha viriba vya kuoteshea miche ya korosho.
Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda akiingia katika eneo la uoteshaji wa miche ya korosho,kushoto ni Wilayani humo kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Christopher Ngubiagai.
Pamela Mollel, Kilwa.
Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI George Kakunda amewataka viongozi wa serikali wilayani Kilwa Mkoani Lindi kuhakikisha wanasimamia vyema upandaji wa miche mipya yazao la korosho hali ambayo itaongeza uzalishaji wa zao hilo kwa wananchi na kuinua uchumi wa Taifa
Hayo aliyasema jana wilayani Kilwa wakati wa ziara yake baada ya kuelezwa kuwa mkakati wa wilaya uliopo ni kuhakikisha wanazalisha na kupanda miche milioni
moja kila mwaka hali ambayo itaongeza mashina ya zao hilo kutoka laki sita yaliyopo na zaidi kutokana na mpango huo kuwa wakudumu
Kufuatia hali hiyo Kakunda alisema ili miche hiyo iote vizuri na kustawi lazima uwepo usimamizi mkubwa kwa viongozi wote wa serikali wilayani humo kuliko kuacha usimamizi kwa wakulima peke yao ambao wanaweza kusababisha kukauka na kushindwa kufikia malengo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: