.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonda kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam. Hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Juma Ameir Hafidh kulia akimkabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu kwa Shule za Jiji la Dar es Salaam. Hafla hiyo ya makabidhiano yamefanyika katika Makao Makuu ya PBZ Mpirani Zanzibar. Kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayuob Mohammed Mahmoud na Mkurugenzi Masoko wa PBZ Said Ali Mwinyigogo
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar, Juma Ameir Hafidh akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni hamsini kwa ajili ya kuchangia Ujenzi wa Vyumba vya Walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marine Thomas.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paulo Makonda akizungumza na kutowa shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo kufanikisha ujenzi wa Ofisi za Walimu wea Shule za Dar es Salaam. Kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kushoto Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir Hafidhi.
Wanahabari wakiwajibika.
Picha ya Pamoja. Bank ya watu Zanzibar (PBZ) imetoa msaada wa hundi yenye thamani ya Shilingi millioni 50 kw Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ikiwa ni kuunga mkono jitihada zake za ujenzi wa ofisi 402 za Walimu Mkoa huo.
RC Makonda ameishukuru Benki ya watu wa Zanzibar kwa kumuunga mkono katika kampeni yake ya ujenzi wa ofisi za Walimu.
Makonda amesema kuwa fedha hizo zitaenda kununua Mifuko 50,000 ya saruji itakayoweza kufyatua tofali zaidi ya 140,000 ambayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kasi ya ujenzi wa ofisi za walimu.
RC Makonda amesema kuwa kilichomgusa kuanza kampeni hiyo ni baada ya kubaini walimu wanafanyakazi katika mazingira magumu.
Benki ya PBZ imeweka dawati maalumu kwenye kila tawi la Bank hiyo kwa ajili ya wananchi wananchi wanaowataka kuchangia ujenzi wa ofisi za walimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Juma Ameir Hafidhi amesema kuwa wameamua kutoa mchango huo kutokana na kazi anayoifanya RC Makonda kutokuwa ya ubabaishaji hivyo wanauhakika fedha walizozitoa zitaifanyia kazi iliyokusudiwa.
Amemuhakikishia RC Makonda kuwa wataendelea kumuunga mkono kwenye shughuli za maendeleo kwa kuwa anafanya maendeleo bila ya kuangalia itikadi za kisiasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: