Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Sadi Kusilawe akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu wa Wilaya ya Ubungo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Sadi Kusilawe akisalimiana na wajumbe wa halmashauri kuu wilaya ya Ubungo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzu (CCM), Wilaya ya Ubungo, Mgonja akimpoke katibu wa chama mkoa wa Dar es Salaam, Sadi Kusirawe.
Baadhi ya madiwani wa chama cha mapinduzi wakimsikiliza katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam.
Kamati ya Watendaji ya CCM wilaya ya Ubungo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Kusalawe amewataka viongozi wa chama hicho kuvunja Makundi na kuacha kabisa swala la maneno ili kufanikisha ushindi wa kishindo katika marudio ya uchaguzi wa Udiwani kata ya Saranga.
Kusilawe amesema hayo alipokuwa anaongea na wajumbe wa halmashauli kuu ya wilaya ya ubungo katika mkutano ulio wakutanisha viongozi hao na kutumia mda huo kuwaasa viongozi hao kuchagua kiongozi bora na atakae kubalika kwa wananchi ili chama kiweze kupata ushindi wa kishindo kwenye marudio hayo ya uchaguzi.
"Uchaguzi ni kama biashara leo tuko saranga, mmepiga kula za maoni jana, kula zile zitakuja kuwaambia kuwa saranga tunakwenda na kuku au bata , tutakapo kwenda watatuambia , nikimaanisha tunapaswa kumchagua mgombea ambae anafaa na anauzika kwa kwa jamii , kwani ukiwa umepita na kuku watu watakuuliza iyo ni biashara ???? Lakini ukibeba bata hakuna atakae kuuliza kwakuwa wanajua unaenda kufuga hivyo hawaulizi bei na sisi tufanye uchaguzi ambao utatupa kiongozi anae pendwa na kukubalika na jamii na majibu tutapata kesho kutwa amesema Kusilawe.
Aidha aliwaasa viongozi kuwa na moyo wa kutunza vitu na kulinda sana mdomo kwani wote tunajua mdomo ni jumba la maneno kuna mda unaweza kuongea kitu ambacho kinajenga au kubomoa, huku akisisitiza kuwa na weledi wa kuchambua mambo punde unapo letewa taarifa yoyote , alizidi kueleza kuwa kiongozi bora hupaswi kuwa na maneno mengi, kiongozi akipenda kuongea sana uyo sio kiongozi bali ni kiwanda cha kuzalisha maneno.
Sambamba na hayo aliwaonya makatibu wa matawi kusimamia vyema vitega uchumi vyote vya chama kwa umakini kwani kuna baadhi ya makatibu wamejibinafsishia vitega uchumi hivyk na kuvimiliki kama vyao kitu ambacho chama hakito kubali wala kufumbia macho vitendo hivyo vya wizi wa mali za chama.
Toa Maoni Yako:
0 comments: