Mgeni Rasmi-Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa ufungua wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira.

Na Mathias Canal, Singida

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu leo Octoba 20, 2017 amefungua Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira juu ya kutoa maoni na mapendekezo juu ya maombi ya Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Wilaya ya Manyoni (WSSA) ya kurekebisha bei za Huduma za Maji Safi.

Akizungumza Wakati wa ufunguaji wa Mkutano huo ulioandaliwa na (EWURA) na kufanyika katika Ukumbi wa Maktaba Mhe Mtaturu Alisema kuwa Maji Ni Huduma muhimu kwa wananchi na uchumi wa Nchi yoyote ile na upatikanaji wake Ni kielelezo tosha Cha ubora wa maisha ya watu wote kwa ujumla hivyo Mkutano huo Ni dira ya maboresho ya upatikanaji maji kwa ajili ya kuwapunguzia kadhia wanayokumbana nayo wananchi ikiwemo umbali kwa ajili ya kuifikia Huduma hiyo.

Alisema kuwa Mwaka 2001 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya kuanzisha chombo chenye jukumu la kudhibiti na kusimamia watoa Huduma (EWURA) katika sekta ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ikiwa Ni pamoja na sekta ya nishati ambapo baadhi ya majukumu yake Ni pamoja na kudhibiti ubora wa Huduma ya Maji nchini kwani awali Huduma za Maji zilikuwa zikisimamiwa na serikali kupitia Wizara ya Maji kwa kutumia Sheria na mikataba mbalimbali.
Baadhi ya wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira wakifatilia Mkutano
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza wakati wa ufungua wa Mkutano wa wadau na wateja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira. (Picha Zote Na Mathias Canal).
Meneja wa EWURA Kanda ya Kati Mhandisi Nobert Kahyoza akiwasilisha hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA wakati wa mkutano wa wadau na watumiaji wa huduma ya maji Manyoni. Wengine ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni Mhe Moses Matonya.

Alisema Uundwaji wa Mamlaka za udhibiti Kama EWURA Ni kielelezo Cha utekelezaji wa kanuni za utawala Bora wenye lengo la kutenganisha majukumu ya kuandaa sera na kusimamia utekelezaji wake kwa upande mmoja, na yule wa udhibiti kwa upande mwingine ambapo serikali imebaki na jukumu la kuandaa sera na kuwasilisha miswada ya Sheria Bungeni, Kusimamia utekelezaji wa sera na mikakati yake, Kuwezesha wananchi kushiriki katika masuala yanayohusu mustakabali wao na kuhamasisha wawekezaji kushiriki katika maendeleo ya sekta na KUJENGA miundombinu.

Mhe Mtaturu Alisema kuwa pamoja na Mkutano huo wa majadiliano Kati ya wadau wa maji Wilayani Manyoni lakini wananchi wanapaswa kutambua kuwa ili kuboresha Huduma za upatikanaji wa maji pia Ni muhimu wananchi kutunza Mazingira kwani maji Yana mahusiano ya Moja kwa Moja na Mazingira.

Mhe Mtaturu Alisema kuwa uharibifu wa Mazingira Ni chanzo Cha upatikanaji hafifu wa maji hivyo wanachi wanapaswa kupanda miti kwa wingi ikiwa Ni pamoja na kutunza vyanzo vya maji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: