Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole (kulia), akimpatia zawadi, mmoja wa wateja wa benki hiyo, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja Oktoba
4, 2017, kwenye tawi la benki hiyo barabara ya Samora jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Huduma kwa Wateja, MCB, Bi. Flora Mbogo, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja, MCB, Bi.Flora Mbogo, na Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole
Viongozi wa MCB, wakiungana na baadhi ya wateja wao kukata keki, ikiwa ni ishara ya kusherehekea pamoja katika kipindi cha wiki ya Huduma kwa Wateka, wkenye tawi la benki hiyo la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole, akimlisha keki, mmoja wa wateja waliohuduria hafla hiyo.
Wafanyaakzi wa MCB, wakiwa katika picha ya pamoja.

NA K-VIS BLOG

Wiki ya kwanza ya Mwezi Oktoba kila mwaka, hutumika kama Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, ambapo taasisi za umma na binafsi, hujumuika pamoja na wateja wao kwa lengo la kuonyesha mahusiano mema katika kutoa huduma na pia kuzunhumzia changamoto za kihuduma kwa mwaka mzima na hatimaye kutafuta njia za kuzitatua changamoto hizo.

Kwa upande wake, MCB iliwaalika wateja wake, na kujumuika nao kwenye tawi la benki hiyo, barabara ya Samora jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi wa benki hiyo walitumia wasaa huo kuwashukuru, wateja lakini pia kuwahamasisha zaidi kutumia huduma za benki hiyo ambazo ni pamoja na kutoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali, wafanyabiashara, wakulima na wananchi kwa ujumla. Hali kadhalika huduma za ATM ambazo zinapatikana Umoja Switch wenye mtandao mpana nchi
nzima.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: