Picha na maktaba.

Na Woinde Shizza, Arusha.

Umoja wa wauza nyama jiji la Arusha (wanjamuco) wametenga kiasi cha shilingi laki tano katika mapato yao kwa ajii ya kuzilipia kaya mbili kwa kila kata zinazoishi mazingira magumu bima ya afya ambayo itawawezesha kupata matibabu bure katika hospitali na zahanati yeyote iliyopo ndani ya jiji la Arusha.

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa umoja huo wa wafanyabiashara wa nyama,   Alex Lasiki alipokuwa akizungumza katika sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja toka kuanzishwa kwa umoja huo.

Alisema kuwa katika kusherehekea kwao mwaka mmoja wao kama wanachama wamekubaliana kuwa watenge kiasi hicho katika mapato yao waliyoyapata kwa mwaka mzima ili wawezeshe familia mbili zenye watu 12 zinazoishi mazingira magumu kupata bima ya afya ijulikanayo kama lita ambayo inasimamiwa na jiji la Arusha.

Lasiki alieleza kuwa kupitia bima hiyo familia hizo zitapata huduma za matibabu bure sehemu yeyote kwenye zahanati au hospitali na kwamba wameamua kufanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida wanayoipata katika jamii wanayoiudumia kupitia biashara yao ya uuzaji wa nyama.

Aidha akielezea changamoto zinazoikabili umoja huo alisema kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa mabucha feki ambayo hayana viwango haswa yaliopo Samunge ambayo yamekuwa yanauza nyama ambazo hazina viwango hivyo kuhatarisha afya za walaji.

Samba mba na hilo waliiomba pia serikali iwajangee kiwanda cha kuchakata ngozi kwani kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya sehemu màalum ya kuuzia ngozi kutokana na serikali kupiga marufuku usafirishwaji wa ngozi hizo nje ya nchi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Diwani wa kata ya Olerian Zakaria Absalum ambae pia ni mfanyabiashara wa nyama amesema kuwa zipo kero kubwa ambazo zinawakabili wafanyabiashara wa jiji la Arusha ikiwemo usafirishwaji wa ng'ombe kwenda nchi jirani ya Kenya ambapo wanaosafirsha hawalipi kodi na wanavyofika mpakani mtu mmoja mwenye leseni yeye ndio analazimika kuingiza mifugo yote kwenda kufanya biashara kwenye ardhi ya kenya bila kuilipia ushuru na hivyo kuisababishia serikali hasara.

Alidai kuwa kutokana na kero hiyo ni vema serikali ikajenga mnada maalum eneo la Namanga ili ijenga ushindani wa wafanyabiashra hao ili kuziba mianya ya wale wanaoingiza mifugo bila kuwa na leseni za biashara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: