Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Suingano Malya wakisaini mkataba wa Mradi wa sita wa kupeleka mawasiliano kwa wote. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini yenye lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini na hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Suingano Malya, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa sita wa kepeleka mawasiliano ya simu kwa wote. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini yenye lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini na hafla hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, (kulia), akimpongeza Mwakilsh wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya, mara baada ya Airtel kusaini mkataba wa sita wa Mradi wa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCAF), jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.
---
UCSAF imesaini makubaliano na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanznia PLC pamoja na makampuni mengine ya simu nchini kwa lengo la kuhakikisha mawasiliano ya simu yanawafikia watanzania wote hadi vijijini. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo kwenye makao makuu ya Mfuko wa mawasilano kwa wote jijini Dar es Salaam,

"Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "Airtel tunasaini mkataba huu kwa lengo la kuendelea kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma za mawasiliano kote nchini zentye ubora na ubunifu wa hali ya juu”

Singano alisema kuwa "uwepo wa mawasiliano haya vijijini utasaidia hasa kutimiza malengo mbalimbali ambayo serikali imejiwekea katika kupanua uchumi wa nchi kwa ujumla katika Nyanja mbalimbali zikiwemo elimu, afya, uboreshwaji wa shughuli za kilimo pamoja na huduma za kibenki kwa maeneo ambayo yako pembezoni mwa nchi.Tunaimani maswala ya uslama kwa watanzania waliopo mipakani yataweza kutatuliwa kwa hara na ufanisi mkubwa kupitia mawasiliano.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: