Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga (Wa pili Kulia) akipokea Tisheti kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zurich Group, Sudi Simba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bima mpya ya Afya, inayojulikana kwa jina la Afya Wote, iliyo chini ya Jubilee Insurance, Zurich Group waanzilishi wa Afya Wote Medical Insurance Scheme, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar esSalaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Jubilee Insurance, Rogation Selengia (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Afya Jubilee Insurance, Kenneth Agunda. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Wakionyesha Vipeperushi na fomu zinazoelezea huduma za Bima hiyo, baada ya uzinduzi huo.
Na Ripota wa mafoto Blog, Dar

WITO umetolewa kwa wananchi wa kipato cha chini na kati kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya mpya unaojulikana ‘Afya Wote’, uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga, alisema kuwa uzinduzi wa mfuko huo wenye gharama nafuu ni kimbilio la wanyonge kutokana na kuwajali wananchi wa aina zote.`
Aidha alisema kuwa wananchi wataona umuhimu wa mfuko huo pindi wanapopatwa na tatizo la ugonjwa na kwa wakati huo wakawa hawana pesa za kukidhi matibabu.
Bima hiyo imelenga zaidi kuwafikia wananchi wote haswa wale waso na kipato kikubwa na wa kipato cha kati ili wote wanufaike na huduma za afya.

Mbanga alitoa wito kwa wananchi wengi kutumia fursa hiyo ili kuweza kuwekeza fedha ambazo wanazitumia kwa matibabu kwaajili ya mahitaji mengine ya kiuchumi.
“Pamoja na kwamba kuna sera mbalimbali za afya zinazozungumza juu ya upatikanaji wa huduma za afya kwa njia rahisi, lakini bado bila bima ya afya wagonjwa wengi watapoteza maisha kwa sababu kuna watanzania wengi ambao hali za kipato chao sio nzuri.
Aidha
alisema asilimia 27 tu, ndio wamejiunga na mfuko hivyo kuna wananchi wengi
ambao hawajajiunga na mfuko huo.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Group na Zurich Insurance Brokers (EA) Sudi Simba alisema, huduma hiyo ilianzishwa mwezi Aprili mwaka jana, lengo likiwa ni kuwasaidia watu wenye kipato cha chini na kati, ambapo kwa kila familia ya watu wanne wataweza kukatiwa bima kwa sh.174,000 tu.

“Watu hawa ni baba, mama na wategemezi wao ambao ni watoto chini ya miaka 18 .

Bima hii kama kuna uhitaji wa kuongeza wengine unapaswa kulipia sh. 100,000 kwa mwaka kwa kila atakaeongezeka,”alisema.
Khadija Kopa na kundi zima la bendi ya TOT wakitoa burudani na kuimba wimbo maalum uliotungwa nao kuhusu Bima hiyo mpya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: