Jeshi la Polisi limewakamata Jumla ya watuhumiwa 267 kwa Makosa mbali
mbali ya kihalifu pamoja na Madawa ya kulevya, Unyang'anyi wa kutumia
Silaha katika Maeneo Mbali Mbali ya Jiji La Dar es Salaam.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Kamanda Polisi kanda Maalum Dar es salaam Saimon
Sirro amesema Operation hii ni endelevu na Jumla ya kete 366 za dawa
zakulevya zimekatwa pamoja puli za bangi 150 na Misokoto ya bhangi 51.
Aidha
Sirro amesema kuwa Operatini Kali ya kuwasaka wahalifu wa Makosa hayo
mbali mbali ikiwemo kosa la kupatikana na Madawa ya kulevya bado
inaendelea na hivyo tunawaomba raia wema waendelee kutoa Ushirikiano
mzuri kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa waalifu.
" Watuhumiwa wote kwa ujumla bado wanaendelea Kuhojiwa Kulingana na Makosa Yao na pindi Upelelezi Utakapokamilika Watafikishwa Mahakamani kwa hatua nyingine zaidi" amesema Sirro.
Pia Kamishna huyo ameongeza kuwa mnamo tarehe 15 Mwezi huu 2017 Majira ya Saa moja Usiku Maeneo ya kiwalani kwa Ally Mboa Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata Silaha Moja aina ya Shotgun ambayo imekatwa kitako na Mitutu na huku namba zake zikiwa zimefutwa.
"Siraha hiyo ilipatikana wakati Askari wakiwa doria katika Maeneo hayo ambapo Waliskia harufu ya bangi na Kuanza kufuatilia ili kubaini ilipokuwa ikitokea na ndipo Ghafla watu wawili wasiofahamika walikurupuka na kupanda pikipiki ambayo haikusomeka namba kisha kuangusha begi moja la mgongoni ambalo lilikuwa na Silaha" amesema Sirro.
Toa Maoni Yako:
0 comments: