Simbu ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu wa Mumbai Marathon ameonyesha umahiri mkubwa katika mashindano hayo hasa ikizingatiwa kuwa mashindano hayo yalikuwa yanashirikisha vinara wengi wa riadha ulimwenguni wakiwemo Muethiopia Kenenisa Bekele wakenya Daniel Wanjiru, Bedan Karoki na Abel Kirui.
Mara baada ya ushindi huo salamu za pongezi zimekuwa zikimiminika huku mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akisema kuwa kampuni yake imeridhishwa sana na ufanisi aliouonyesha katika mashindano hayo. Amesema uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo katika kumdhamini Simbu umezaa matunda kwani kiwango cha mwanariadha huyo kimekuwa kikiimarika siku hadi siku. “Tumefurahishwa sana na kiwango alichoonyesha Simbu kwenye London Marathon. Hii ni ishara nzuri sana na tunaamini atafanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya riadha ya Dunia yatakayofanyika jijini London mnamo mwezi Agosti mwaka huu”
Kwa upande wake, meneja wa mwanariadha huyo Francis John amesema kuwa ameridhishwa na kiwango alichoonyesha Simbu na kwamba punde tu atakaporejea wataanza maandalizi kwa ajili ya ushiriki wake katika mashindano ya Dunia yatakayofanyika mwezi agost mwaka huu.
Katika mashindano hayo nafasi ya kwanza imechukuliwa na Mkenya Danie Wanjiru (2:05:48) akifuatiwa kwa karibu na Kenenisa Bekele (2:05:57) na Bedan Karoki (2:05:41).
Toa Maoni Yako:
0 comments: