Askofu wa kanisa la Pentecote Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania Dkt. Rejoice Ndalima akifaya maombi.
Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo Iringa Paul Mtakwimwa.
Askofu wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania Dkt. Rejoice Ndalimaakiwaombea waumini wake na Taifa.
Wachungaji wakiwa katika maombi.
Askofu wa kanisa la Pentecoste Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania Dkt Rejoice Ndalima akimsimika mchungaji Paul Mtakimwa na mkewe.

Na MatukiodaimaBlog

ASKOFU mkuu wa kanisa la Pentecote Tumaini Gospel Centre nchini Tanzania Dkt. Rejoice Ndalima amewataka viongozi wa dini nchini kutumia nyumba za ibada kumwombea Rais Dkt John Magufuli na kuliombea Taifa badala ya kutumia nyumba hizo kusema kuumbua viongozi wa serikali.

Kuwa kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli katika nchi hii si ya kubenzwa makanisani na wachunguzaji ama viongozi wengine wa dini bali ni kazi ambayo inapaswa
kuombewa zaidi ili Taifa lizidi kubarikiwa.

Askofu huyo ametoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo Mtwivila mjini Iringa pamoja na kumsimika mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Paul Mtakwimwa kuwa hivi sasa
heshima ya nyumba za ibada imeanza kupoteza uwepo wa Mungu kutokana na baadhi ya watu kutumia nyumba za ibada kama sehemu ya masengenyo na utapeli jambo ambalo si sahihi.

Alisema kitendo cha baadhi ya makanisa nchini kutumiwa na wanasiasa ama vikundi vya watu kuishambulia serikali ama kufanya utapeli wa fedha za waumini wao kwa kuwatoza fedha kama malipo ya huduma wanayoitoa si sahihi na si kazi ya nyumba za ibada hasa makanisa .

Pasipo kutaja majina ya makanisa yaliyogeuzwa majukwaa ya wanasiasa na baadhi ya watu waovu ama yanayofanya utapeli wa pesa kwa waumini wake alisema kuwa yamezuka makanisa ambayo kimsingi hayakupaswa kuitwa makanisa ili yalipaswa kuwa ni vyama vya siasa ama nyumba za waganga wa kienyeji kwa maana ya wapiga ramli.

“Baadhi ya makanisa yamepoteza sifa ya kuitwa ni makanisa maana wanafanya vituko vya ajabu sana ndani ya madhabahu ya Mungu … wapo wanaotumiwa na wanasiasa kueneza siasa makanisani na kila siku wao ni kuwa ni wachonganishi dhidi ya serikali na watu wake na wengine wamegeuka watabiri wa uongo na watenda miujuzi hatarishi kwa jamii“

Alisema kuwa kazi ya viongozi wa dini ni kuhubiri neon ili watu wote waweze kumjua Mungu na sio kuhubiri siasa ama kuifundisha kazi serikali ya kufanywa wakati si jukumu la kanisa kuwa iwapo watu wote watamjua Mungu watafanya kazi ya kuhudumia jamii kwa kutanguliza hofu ya Mungu hivyo hakutakuwa na ufisadi , wizi ama watumishi hewa hivyo kazi ya kanisa ni kuwafanya watu waijue kweli na kweli iwe ndani ya mioyo yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: