Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kinachofanyika Mkoani Dodoma.

Na Lorietha Laurence - Dodoma.

Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  kwa kuanzisha mawasiliano ya kimkakati  yatakayosaidia kuhamasisha na kusukuma agenda muhimu za kitaifa ikiwemo kuelekea uchumi wa viwanda,vita dhidi ya madawa ya kulevya na uzalendo.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akifungua mkutano wa 12 wa Maafisa Mawasiliano Serikalini Mjini Dodoma ambapo aliwasisitiza kuwa kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi.

“Maafisa Mawasiliano ni daraja muhimu katika kutoa taarifa kwa umma na kujenga taswira ya Serikali ili kufikia malengo yaliyowekwa hivyo basi kwa kufahamu jukumu hili ni wajibu wa kila Afisa kuwa mstari wa mbele katika kuhabarisha umma kuhusu mkakati wa maendeleo uliowekwa na serikali“alisema Waziri Nape.

Aliongeza kuwa Maafisa Mawasiliano wahakikishe baada ya kikao kazi hicho wanatoka na mpango mzuri wa mawasiliano ya kimkakati ili kurahisisha utoaji na upatikanaji wa habari na taarifa muhimu kwa wananchi utakawasaidia kujua mpango wa maendeleo na utekelezaji wake.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mhe. Elizabeth Simon Kitundu ameishukuru Wizara kuandaa mafunzo kwa Maafisa Mawasiliano Serikalini na kuyafanyia Mkoani Dodoma kwani kwa kufanya hivyo itarahishisha mfumo wa kimawasiliano na kutangaza fursa zilizopo Mkoani humo.

“Mmekuja kpindi kizuri sana ambapo tayari  serikali imeashaanza kuhamishia Wizara na Taasisi zake katika mkoa wetu ukizingatia Mji wa Dodoma una fursa nyingi za uwekezaji, na tayari huduma muhimu za msingi kama vile barabara, hospitali, huduma za maji,makazi na shule zinazidi kuimarishwa “ alisema Bibi. Elizabeth.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw.Innocent Mungy aliahaidi kuufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri Nape ili kuhakikisha wanaisemea Serikali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: