Mchungaji Geofrey Kaijunga akitoa mahubiri katika ibada ya Jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga.
Ibada ya Jumapili katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria ikiendelea
Mchungaji Jackson Maganga wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, akiwakaribisha kanisani viongozi wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania
Afisa Programu kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania Severin Edward akiteta jambo na Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS)Josephat Torner
Kushoto ni Mkurugenzi wa wanawake,Watoto na Diakonia katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Martha Ernest Ambarang'u akiwatambulisha viongozi kutoka TAS.Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Programu kutoka TAS Severin Edward, akifuatiwa Happiness Ngaweje na afisa mahusiano na habari (TAS)Josephat Torner
Afisa Mahusiano na Habari kutoka TAS,Josephat Torner akizungumza kanisani

Waumini wakimsikiliza Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner
Afisa Mahusiano na habari kutoka chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) Josephat Torner akiendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino huku akiitaka jamii kutoa ushirikiano wa dhati katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino.
Waumini wakipa somo kuhusu masuala ya ualbino.
Mchungaji Jackson Maganga wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria akieleza namna kanisa hilo linashiriki katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu wenye ualbino
Mchungaji Jackson Maganga akizungumza kanisani.
Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani.
Mchungaji Goodluck Mosha akizungumza jambo kanisani.
Wachungaji wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria.
Viongozi wa TAS wakiwa kanisani.
Waumini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kanisani.
Waumini wa kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria wakiwa nje ya kanisa baada ya ibada kumalizika.
Viongozi wa TAS wakiondoka katika kanisa la KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria.
---
Chama
cha watu wenye ualbino nchini (Tanzania Albinism Society-TAS) kimeanza
kampeni ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ualbino katika nyumba za ibada
ambapo leo viongozi wa chama hicho taifa wametoa elimu katika kanisa la
KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Dayosisi ya Kusini Mashariki ya
Ziwa Victoria lililopo mjini Shinyanga.
Viongozi hao
wakiongozwa na Afisa Mahusiano na Habari kutoka TAS ,Josephat Torner
wametoa elimu kuhusu mambo ya ualbino kanisani hapo wakati wa ibada ya
Jumapili leo Machi 26,2017.
Akizungumza kanisani hapo
Torner alisema kampeni hiyo inalenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu
masuala ya ualbino kwa viongozi wa dini na waumini wao na wanaendelea
pia kutoa elimu hiyo kwa makundi mengine ya watu katika jamii wakiwemo
waganga wa kienyeji.
“Tumeona vita hii tunayopambana
nayo bila kumjua hasa adui ni nani,ni vyema elimu iwafikie watu wengi
zaidi na tunaamini kupitia nyumba za ibada jamii itakuwa na uelewa wa
kutosha juu ya masuala ya ualbino ili kukabiliana na tatizo la mauaji ya
watu wenye ualbino na hata vitendo vya kufukua makaburi ya watu wenye
ualbino vinavyoendelea kujitokeza nchini”,alieleza Torner.
Alisema
bado watu wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu masuala ya ualbino hali
inayosababisha kuongezeka kwa unyanyapaa ambapo sasa hata wamiliki wa
nyumba za kupanga wanawanyima vyumba watu wenye ualbino wakihofia kupata
matatizo.
“Nyumba za ibada zina watu wengi,tutapita
kwenye makanisa na misikiti kutoa elimu hii ili viongozi na waumini
waelewe hasa maana ya ualbino ili tuungane pamoja kutokomeza vitendo vya
kikatili dhidi ya watu wenye ualbino”,aliongeza Torner.
“Kutokana
na imani potofu katika jamii watu wenye ualbino wanaishi kwenye vituo
maalum,wanaishi kwa hofu kubwa ya kuuawa na sasa kuna baadhi ya watu
wameanza kufukua makaburi ya watu wenye ualbino hivyo kunahitajika
jitihada zaidi katika kupambana na ukatili huu”,alisema Torner.
Alisema
mbali na jitihada zinazofanywa na serikali katika mapambano dhidi ya
ukatili huo ni vyema jamii ikatoa ushirikiano katika kupiga vita vitendo
hivyo vya kikatili.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi
wa kanisa hilo,Mchungaji Jackson Maganga alisema kanisa hilo lina
programu nyingi za kutoa elimu kwa waumini wake juu ya vitendo vya
ukatili kwa watu wenye ualbino na kwamba kanisa hilo liko tayari
kushirikiana na chama hicho katika mapambano dhidi ya ukatili kwa watu
wenye ualbino.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Toa Maoni Yako:
0 comments: