Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza kwenye kikao cha pamoja baina yake na viongozi wa mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro wa mipaka uliopo kati ya wilaya za kilindi na kiteto ili kuona namna ya kuumaliza
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella akizungumza kwenye kikaohicho.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Dokta Joel Bendera akizungumza kwenye mkutano huo kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala
Baadhi ya wenyeviti wa halmasahuri zote mbili na wakuu wa wilaya za Kiteto na Kilindi wakifuatilia kikao hicho
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Sauda Mtondoo akifuatilia majadiliano hayo

WAZIRI wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amewataka viongozi kutoka Mkoa wa Manyara na Tanga kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kumaliza mgogoro wa mpaka katika ya Wilaya ya Kilindi na Kiteto kwa kuhakiki upya mpaka huo kupitia GN namba 65 ya mwaka 1961.

Lukuvi aliyazungumza hayo jana Mkoani hapa alipokutana na viongozi  kutoka Mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili ambapo aliwataka washirikiane kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kama Waziri Mkuu alivyoagiza pindi alipofanya zira yake mkoani hapa.

Aidha alisema kupitia Wizara ya ardhi imeteuwa wataalamu wa ardhi ambao hawatatoka kati ya Mikoa yenye mvutano wa mgogoro huo ili kujenga imani kwa wananchi na watakuwa na jukumu la kuhakiki upya mpaka huo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

"Timu ya wataalamu kutoka wizara yangu imekwishaundwa kwa kufanya kazi  hiyo mategemo ya utekelezaji wa majukumu hayo tunatarajia kuanza rasmi machi 1 mwaka huu na zoezi hili litadumu kwa mwezi mmoja tu na wala hakuna ubabaishaji"Alisema Lukuvi.

Alisema hakuna mpaka mpya utakaokwenda kupimwa kati ya Wilaya hizo  mbili zaidi ya kuhakiki ule wa awali ambao unatokana na ramani ya mwaka 1961,zoezi hili la uhakiki lazima wananchi na viongozi watambue kuwa linafanyika kwa mara ya tatu na litakuwa la mwisho.

Pia aliwataka viongozi wote kuanzia ngazi ya mkoa mpaka Kijiji kushiriki vema katika zoezi hilo ili kuweza kujadiliana hasa pale panapotokea mapungufu na waache kutatua mgogoro huo huku wakiwa na matakwa yao binafsi na kufanya hivyo hakutamaliza mgogoro huo zaidi ya kuuwongeza.

"Kama kuna viongozi wanamatakwa yao basi watambue hawatapata nafasi na tayari tulishapokea agizo kutoka Waziri Mkuu na kinachotakiwa hapa ni utekelezaji wa kumaliza mgogoro huo"Alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Tanga Martin Shigela alisema jukumu kubwa lililopo mbele yao ni kutoa ushirikiano kwa timu iliyoundwa na Wizara hiyo na kuhakikisha wanafanikiwa kumaliza mgogoro huo kwa wakati kama Waziri alivyoagiza.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera alisema lazima viongozi washirikiane kwa pamoja kutatua mgogoro huo ambao umekuwa ni tatizo kwa Wilaya hizo mbili na kupongeza hatua ya Serikali ya uhakiki upya hasa kwa kufuata GN ya namba 65 ya mwaka 1961 kama alivyoagiza Waziri Mkuu na si vinginevyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: