Wachezaji wa Timu ya Ngaya ya nchini Comoro wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga utakaofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa awali uliofanyika Comoro Yanga ilishinda bao 5-1.
Picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili.
Mmoja wa viongozi wa timu hiyo (kushoto), akitoa maelekezo kabla ya kuondoka uwanjani hapo.
Wachezaji wa timu hiyo wakiingia kwenye gari kuelekea hotelini walikofikia.

Na Dotto Mwaibale

KIKOSI cha Timu ya Ngaya kutoka nchini Comoro kimewasili nchini kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Yanga katika dimba litakalofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo imewasili leo saa saba na nusu mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), huku ikiwa imeongozana na baadhi ya viongozi wake.

Mara baada ya kuwasili timu hiyo ilipokelewa na wananchi wa nchi hiyo wanaoishi hapa nchini hata
hivyo viongozi wa timu hiyo hawakuwa tayari kuzungumza chochote na wanahabari badala yake walipiga picha ya pamoja na wachezaji na kisha kupanda kwenye magari na kuondoka.

Katika mchezo wa awali uliofanyika nchini humo Yanga iliibuka kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu hiyo.

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kuwa waamuzi wake wanatarajiwa kufika leo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: