Mhe,Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi.
Picha ya pamoja kati ya waheshimiwa majaji kanda ya Arusha na Kilimanjaro, Wakwanza kulia ni mhe,Jaji Dkt.Modesta Opiyo, Wakwanza kushosto ni mhe. Jaji Salma Maghimbi,akifuatiwa na aliyeko kushoto kwake mhe. Jaji Sekela Mushi, akifuatiwa na mhe,Jaji mstaafu Fatuma Hamis Masengi wakiwa na majaji wengine pamoja na waheshimiwa mahakamu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mhe. Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi akiwa na waheshimiwa mahakimu wa mahakama ya mwanzo (waheshimiwa mahakimu hao wamelelewa na mhe. Fatuma Masengi).
Picha ya pamoja ya waheshimiwa majaji pamoja na mawakili wa serikali,na wale wa kujitegemea.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na Vero Ignatus.
Sherehe za kumuaga aliyekuwa Jaji mfawidhi wa mahakam kuu kanda ya Arusha Mhe. Fatuma Hamis Masengi, zimefanyika leo katika mahakama kuu ya ndanda hiyo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo majaji, mahakimu,mawakili wasajili wa mahama watendaji pamoja na wageni
waalikwa.
Sherehe hizo zimeanza majira ya saa asubuhi katika mahakama ya wazi ambapo Jaji Fatuma alianza kufanya kazi mnamo mwaka 1974 katika mahakama ya mwanzo na kuendelea kuitumikia mahakama hadi alipoteuliwa kuwa jaji mfawidhi mahakama kuu.
Amewataka majaji na mahakimu pamoja na wale wote wanaofanya kazi za kimahakama wafanye kazi kwa kumtegemea Mungu huku wakijua kazi yeyote ina changamoto zake hivyo ni vyema kufanya kazi kwa weledi zaidi na kwa kuzingatia sheria inavyosema,wakimtendea haki kila mtu kwa stahiki.
Amewataka wanawake kutokukata tamaa huku akisema kuwa wanawake wanaweza kuliko wanaume japo kuwa wakati mwingine wanaume wanaona kama vile wanawake ni wanyonge lakini mwanamke anaweza pale ambapo anasimama kwa nafasi yake na kulitumikia kusudi kwa wakati na weledi.
"Wanawake wenzangu msikate tamaa na kujiona wewe ni dhaifu ,tunaweza msibweteke unapopata nafasi itumie vizuri bila kuaharibu taratibu zilizowekwa, fanya kazi kwa bidii na jamii itaona juhudi zako ,wanawake tunaweza" alisema masengi.
Aidha Jaji Fatuma amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha kwa wakati wote ambapo amekuwa akifanya kazi yenye majukumu mazito, amezishukuru Asasi za kiserikali na zile
zisizo za kiserikali,amewashukuru wale wote walioshirikiana nae katika kipindi chote alichokuwa akitimiza majukumu yake ya kikazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: