Nabii mkuu mheshimiwa Dkt. Geordavie akiombea bajeti mbalimbali za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii.

Na Woinde Shizza, Arusha.

Watanzania nchini wametakiwa kusaidia Jamii ya watu wasiojiweza ikiwemo walemavu,watoto yatima pamoja na wazee ili waweze kupata mahitaji yao na kuondokana na umasikini uliokithiri.

Hayo yameelezwa na Baadhi ya Wananchi waishio katika kata ya Kisongo mkoani Arusha ambapo walisema kuwa jamii ya wahitaji imekua ikiishi katika mazingira magumu hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa anawasaidia jamii hiyo.

"Katika jamii kuna watu wengi wakiwemo watoto wanatoto na watu wasio jiweza ambao wanakaa katika mazingira magumu mno hivyo ni wajibu wetu sisi kuwasiaidia wale ambao awajiwezi ,mtu ukiwa na uwezao kidogo unatakiwa ujijengee tabia ya kuwasiaida hawa wasio jiweza" alisema Sekela Tondolo.

Kwa upande wake Mkazi mwingine wa kata ya Kisongo Wiliam James Alisema kuwa jamii ya wasiojiweza imekua ikisahaulika mara kwa mara hivyo ni jukumu la kila Mwananchi kuhakikisha kuwa anafanya kitu kwa ajili ya jamii yake kitakacholeta mchango ambao ni chanya na kuwawezesha kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo kimaisha.

Kwa upande wake Mheshimiwa Nabii Mkuu Dkt. Geor Davie wa Huduma ya Ngurumo ya Upako katika ibada ya makusanyo ya vitu na fedha kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji alisema kuwa taasisi za dini hazina budi kujikita katika kuwasaidia wahitaji na wasiojiweza ili kuwa na taifa imara na endelevu.

"Ni wajibu wa taasisi za kidini, makampuni mbalimbali, hata watu binafsi ambao wanauwezo kuweza kusaidia watu hawa wenye mahitaji na walae wasio jiweza ili nao wajisikie vyema na kuona nao ni sehemu ya watu kama wengine" alisema Geor Davie.

Huduma hiyo inautaratibu endelevu wa kila mwaka wa kupeleka mahitaji kwa wato wasiojiweza pamoja na kuwawezesha kiuchumi kaya zilizoathiriwa na umasikini kwa kiasi kikubwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: