Mkurugenzi wa tasisi ya fedha ya Brac, Mahufuzii Ashrafu , akizungumza na baadhi ya wabunifu katika mkutano huo
Mbunifu wa mashine ya kukamua matunda kutoka mkoa wa Songwe , Yohana Mwanzyunga(Fulana ya Mistari) akiwaonyesha washiriki wengine mtambo wa kukamua matunda.
Baadhi ya washiriki wakiangalia mashine ya kupukucha halizeti
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
Jumla ya Vikundi 16 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini vinavyojiusisha na masuala ya kilimo vimeweza kukutanishwa na Tasisi za kifedha na mabenki hili waweze kuwezeshwa kama mpango wa tasisi ya Land O Lakes.
Akiazungumza na Globu hii Mshauri wa biashara bunifu kutoka tasisi hiyo ,Renalda Lema amesema kuwa katika vikundi hivyo 16 wameweza kuwakilishwa na watu wawiliwawili hili waweze kuwasilisha ubunifu wao kwa tasisi hizo hili waweze kupata fursa ya kupanua biashara yao.
“umeweza kuona wabunifu walivyoweza kutengeza mashine mabalimbali amabzo zitaweza kumuondoa mkulima kutoka sehemu hadi nyingine hasa katika serikali hii ambayo inahamasisha uchumi wa viwanda hivyo sisi tumeona uchumi wa viwanda auwezi kufanikiwa bila ya kuanza kuwawezesha wakulima katika hatua ya mwanzo kabisa” amesema Renalda.
Ametoa wito kwa wadu na tasisi mbalimbali ambazo zinahitaji kuwawezesha wakulima hao kwa namna moja hama nyingine waweze kuwasiliana na tasisi ya Land O’ Lakes waweze kuwakutanisha na wakulima hao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: