Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi walizopeleka katika kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Upendo cha mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro,(KCRI) Profesa Blandina Mbaga akisalimiana na Msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo cha mjini Moshi Sister Yasinta walipofika kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Prof Blandina Mbaga akizungumza na Mkurugenzi wa fedha Hosptali ya Rufaa ya KCMC,Hilda Mungure (katikati) na Elizabeth Msoka.
Msimamizi wa Kituo cha Upendo cha mjini Moshi ,Sista Yasinta Diwi akiwaongoza watoto wanaolelewa katika kituo hicho kuwaimbia wageni waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya kutoa zawadi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) akitoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho.
 Mfanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Anita akiwapa vipande vya Keki watoto wanaolelewa katika kituo cha Upendo cha mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Prof Blandina Mbaga akizungumza muda mchache kabla ya kuwaona watoto waliolazwa katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
 Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakitoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika wodi za watoto Hosptali ya Rufaa ya KCMC. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: