Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Sheikh Sherali Champsi mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,
Baadhi ya Viongozi na waalikwa mbali mbali wakiwa katika Sherehe ya kuadhimisha Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein(katikati) akiwa na wake wa Viongozi mbali mbali na Wananchi wakiwa katika sherehe za maadhimisho ya Maulid ya kuzalia Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) katika Maulid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuangalia Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akitia ubani kama ishara ya Kuyafungua Maluid matukufu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) Sherehe zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Waislamu na Wananchi waliohudhuria katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Ustadh Ali Muombwa Hassan wa Chuo cha Kiislamu akitoa Tafsiri ya Qur'aan Tukufu ya Suratul Touba (Aya 128 hadi 129) iliyosomwa katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Wanafunzi wa Madrassa Hidayatul Munineema na Nurul Islamia ya Mpendae Mjini Unguja wakisoma Qaswida YaRabii Swali katika sherehe tukufu ya Maulid ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Ustadh Mohamed Khamis Rashid wa Kiweani Pemba akisoma maulid Barzanji mlango wa kwanza katika sherehe tukufu ya kuzalia kwa Mtume Muhammad (S.A.W) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akifukiziwa Udi baada bya kutiliwa marashi wakati kumswalia mtume Muhamad (S.A.W) wakati sherehe ya maadhimisho ya maulid
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mw3anamwema Shein (katikati) pamoja na Wake wa Viongozi wakisimama kumswalia Mtume (S.A.W) wakati wa Maulid hayo.
Mashekhe mbali mbali na wananchi waliohudhuria katika sherehe za maadhimisho ya Maulidi ya kuzaliwa Kiongozi wetu Mtume Muhammad (S.A.W) wakisimama kumswalia jana katika sherehe zilizofanyika katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akipookea Zawadi ya Qaswida ya mwaka kutoka kwa Sheikh Sherali Champsi, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) wakati wa sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Sheikh Mohamed Kassim akitoa Khutba yake wakati wa sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja.
Wanamadrssa kutoka Mtendeni Mjini Unguja wakisoma Maulid ya Hom wakati wa sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)
Akina mama waliojitokeza katika sherehe za maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W)
Wanafunzi wa Madrassa mbali mbali na Wananchi wakiwa katika sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Sheikh Sherali Champsi Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe ya maadhimisho ya maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) baada ya kumalizika kwa sherehe hizo zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Unguja,(kushoto) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud.Picha na IKULU, Zanzibar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: