Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande akimkabidhi mlezi wa kituo hicho mafuta ya kula. Wengine ni wafanyakazi wa Multichoice Tanzania na watatu kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Alpha Joseph.
Ofisa wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Johnson Mshana (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kulia), akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo. Kushoto ni mama mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto), akimkabidhi sare za shule mama mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf.
Watoto wa kituo hicho wakishangilia baada ya kukabidhiwa msaada huo.
Mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf (kushoto), akimuonesha nguo zinazotengenezwa na kituo hicho kupitia mradi wao wa ushonaji ambao kwa kiasi kikubwa umetokana na msaada kutoka katika kampuni hiyo ya Multichoice Tanzania.

Multichoice Tanzania imefanya ziara yake kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo mnamo tarehe 22 Desemba. Kusudi la ziara hiyo, ilikuwa kutoa msaada msimu huu wa krismasi kwa watoto hao. Baadhi ya viongozi, wafanyakazi wakiongozwa na mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania Ndugu Maharage Chande, waliwasilisha zawadi hizo kwa mlezi wa kituo hicho, aitwaye Mama Kuruthum Yussuph.

Multichoice Tanzania ilimkabidhi mlezi wa kituo cha Al-Madina (Bi Kuruthum) vifaa mbalimbali vya kuwasaidia watoto hao katika mahitaji yao ya kila siku . Miongoni mwa zawadi zilizotolewa ni vyombo vipya vya kulia chakula, nguo, vyakula, sare za wanafunzi wa shule za msingi, vifaa mbalimbali kwa ajili ya mahitaji ya kila siku, pamoja na kodi ya pango, Jumla ya mahitaji yote yaliyokiabidhiwa leo ikiwa ni ya sh. Milioni tano (5).

Mnamo mwezi wa sita (6) mwaka huu, Msimu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Multichoice Tanzania ilitembelea tena kituo hiki na mojawapo ya mahitaji yaliyopelekwa ilikuwa ni Vyerehani vinne (4). Siku ya leo mlezi wa kituo Bi Kuruthum Yusufu ameonyesha eneo la biashara la ushonaji liloanzishwa baada ya kukabidhiwa vyerehani vile (Pichani). Biashara hii inawasaidia kuwapatia kipato cha kila siku ambacho husaidia kutimiza baadhi ya mahitaji muhimu ya watoto hawa.

Bi Kuruthum na watoto wa kituo cha Al-Madina walitoa shukurani zao za dhati kwa msaada uliyotolewa na Multichoice Tanzania katika kuwasaidia kutekeleza majukumu yao ya kila siku. Multichoice Tanzania imekuwa ikisaidia kituo hicho tangia mwaka 2009, mpaka sasa.

Akiwa anakabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji Mheshimiwa Maharage Chande alisisitiza juu ya umuhimu wa kushirikiana na kituo hicho katika kuwawezesha watoto kusonga mbele kwani ndiyo taifa la kesho, na kila mmoja wetu ana wajibu wa kujitolea kwa namna moja au nyingine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: