Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi NBAA. Profesa Isaya Jairo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida (katikati mwenye tuzo), akiwa na wafanyakazi wenzake baada ya kutunukiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa NBAA.
Na Dotto Mwaibale.
MFUKO wa Pensheni wa LAPF, umetunukiwa tuzo ya kuwa kinara katika utunzaji wa mahesabu dhidi ya mifuko mingine ya hifadhi ya jamii nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Elyudi Sanga baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa mfuko huo, John Kida, alisema kwao ni mafanikio makubwa kwa kupata tuzo hiyo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe, alisema kuwa wanachama wao wanatakiwa kuendelea kuwa na imani na mfuko wao na kuwa fedha zao zipo kwenye mikono salama.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Pius Maneno, alisema makampuni na taasisi 56 zilishiriki katika mashindano hayo kwa mwaka huu ambapo waligawanywa katika makundi 12 kulingana na huduma wanazozitoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: