Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Simba Sports iliyokuwa ikiitwa Senderland, Athur Mwambeta amewaomba wadau mbalimbali wa mchezo wa soka nchini na Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsaidia kupata chombo cha usafiri kitakachomtoa sehemu moja mpaka nyingine mara baada ya kukatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi yanayomkabili. 

Mwambeta amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na Globu ya jamii katika hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo amelazwa katika jengo la Kibasila ward namba 11, ambapo anaendelea na matibabu mara baada ya kukatwa mguu ijumaa iliyopita.

"Nimeugua maradhi haya pindi tu nilipoacha kucheza mpira hali iliyopelekea kukatwa mguu wangu wa kwanza mwaka 2015 na mwaka huu ijumaa iliyopita ndipo nilipokatwa mguu wangu wa pili na kubaki kama hivi mnavyoniona, kwani siwezi tena kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama ilivyokuwa awali hivyo kwa yoyote anaeweza kunisadia naomba ajitokeze " amesema Mambeta.

Amesema kuwa anaomba wadau kumchangia kupitia nambari hii 0714435312 ili aweze kujikwamua katika changamoto mbalimbali za kimaisha.

Pia alitoa wito kwa wapenzi na wanachama wa CCM kujitokeza kumsadia kwani wao ni moja ya watu waliokuwa wahamasishaji wakubwa kupitia TANU mpaka ilipozaliwa CCM walitumia mpira kama sehemu ya hamasa.

Wachezaji wa zamani wakiongozwa na Kitwana Manara wakimjulia hali,Athur Mwambeta,ambaye amekatwa miguu yote miwili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: