Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli amlaki mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno kwa viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama mara baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimzawadia kinyago cha Kimakonde cha "Umoja" na picha ya kuchora ya tembo na Mlima Kilimanjaro na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara baada ya kiongozi huyo kuwasili kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akisalimiana na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali za Afrika nchini mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa na mizinga 11 mara baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akikagua gwaride rasmi i mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtambulisha Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu kwa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe kassim Majaliwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni ya leo Novemba 27, 2016.---
Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu leo tarehe 27 Novemba, 2016 majira ya jioni amewasili hapa nchini kwa ziara ya kiserikali ya siku 3 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais Lungu amepokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kulakiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hapa nchini pamoja na wananchi. Akiwa uwanjani hapo Rais Lungu amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Kesho tarehe 28 Novemba, 2016 Rais Lungu ataendelea na ziara yake hapa nchini ambapo pamoja na kutembelea miradi ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia ikiwemo TAZARA na TAZAMA, atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, atashuhudia utiaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia na jioni
atahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Magufuli kwa ajili yake Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe. Idriss Deby Itno leo tarehe 27 Novemba, 2016 majira ya alasiri amewasili hapa nchini kwa ziara kikazi ya siku 2.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Idriss Deby Itno akiwa na Mkewe Mama Hinda Deby amepokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli na kisha kulakiwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe.
Kassim Majaliwa na wananchi. Jioni hii, Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Rais Idriss Deby Itno Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Novemba, 2016
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: