Siku moja nilichukua taxi nikiwa naelekea uwanja wa ndege. Dereva huku akiendesha kwa ustaarabu sana mara ghafla pasipo kutegemea gari ya taka ikajitokeza mbele yetu kutokea nje ya barabara. Dereva wa taxi kwa umakini na neema ya Mungu akalikwepa gari hilo na ilikuwa kidogo agonge gari zingine mbele yetu. Pasipo kutegemea dereva wa gari la taka akaanza kufoka na kutoa matusi kwa kelele kubwa!
Katika hali ya kushangaza dereva wa taxi alitabasamu na kuwapungia mkono waliokuwa kwenye gari la taka na ndipo kwa mshangao nilimuuliza; "Inakuwaje ufanye hivyo wakati walitaka kutuua na hata kuharibu mali yako?" Akajibu kwa upole akinitazama kwa tabasamu akasema. “Katika maisha yetu, kuna watu wako kama gari la taka. Wamejaa misongo, hasira, maumivu, wamechoka kifikra, kiuchumi na kimaisha, na wamejaa masikitiko mengi. Watu hao takataka zao zinazopowazidi hutafuta mahali pa kuzitupa na haijalishi mazingira wanakozitupia. Hivyo jIfunze kutogombana nao. Wapungie mkono, wape tabasamu, songa mbele. Haikupunguzii kitu. Wala usiruhusu takataka zao zikupate."
Uliumbwa kuyafurahia maisha. Usiyafupishe kwa kuamka asubuhi na kinyongo, na hasira, na ghadhabu kwa sababu ya mtu fulani. Yesu anatushauri; “Lakini nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.” (Luka 6:27-28)
Watafiti wanasema 10% ya maisha ni vile ulivyoyatengeneza lakini 90% ya maisha ni vile unavyochukuliana nayo. Jifunze kuchukuliana na maisha kuliko vile unavyoyatengeneza huku ukimtegemea Mungu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: