Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za wizara (hawapo pichani), wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kulia ni Naibu Waziri Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za wizara (hawapo pichani), wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kulia ni Naibu Waziri Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
 Wakuu wa Taasisi na Idara za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi; Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Wakimbizi pamoja na wakuu wa vitengo wizarani hapo wakimsikiliza Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, wakati kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Idara zake. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam. 
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: