Mkurugenzi wa asasi ya msaada wa kisheria ya LASWA mkoa wa Iringa Francis Mwilafi akizungumza wakati wa uzinduzi wawa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa akina mama wajawazito na watoto,warsha iliyoshirikisha madiwani na watendaji wote wa kata za wilaya ya Kilolo, kulia ni meneja wa LASWA Oscar Lawa.
Katibu tawala wa wilaya ya Kilolo Yusuph Msawanga akizindua wa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa akina mama wajawazito na watoto.
Madiwani wa Halmashauri ya Kilolo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katibu tawala wa Kilolo Yusuph Msawanga wa nne kutoka kulia mara baada ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa akina mama wajawazito na watoto.
Mkurugenzi wa Laswa akieleza lengo la mradi huo.
Watendaji wa kata zote za Kilolo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katibu tawala wilaya ya Kilolo
Katibu tawala wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Yusuph Msawanga (wa nne kulia waliokaa) akiwa na mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na huduma ya msaada wa kisheria wa bure kwa wananchi mkoani Iringa Francis Mwilafi kushoto kwake na baadhi ya wafanyakazi wa LASWA na madiwani mara baada ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa akina mama wajawazito na watoto.
Na Matukiodaima Blog.
MKUU wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah ameiomba asasi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na msaada wa kisheria ya LASWA kusaidia kutoa elimu zaidi kwa wananchi ili kuwezesha jamii wilayani humo kujua sheria na kukomesha mimba za utotoni na unyanyasaji kwa wanawake.
Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa kuimarisha huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa haki kwa wote hasa akina mama wajawazito na watoto, jana mkuu huyo aliyewakilishwa na katibu tawala wa wilaya hiyo Yusuph Msawanga alisema kuwa mradi kuzinduliwa kwa mradi huo katika wilaya ya Kilolo iwe ni mwisho wa jamii kunyanyasika na iwe mwisho wa mimba za utotoni.
Alisema kuwa jamii kutokana na kutojua sheria ama wajibu wao kwa watoto kumekuwepo na changamoto za watoto wa kike kukatishwa masomo yao kutokana na mimba za utotoni ama wato kuwatorosha kwenda kufanya kazi jambo ambalo kisheria ni kosa.
Hivyo alisema kutokana na mafunzo hayo yametolewa kwa madiwani na watendaji wa kata zote za wilaya ya Kilolo na LASWA kutoa wasaidizi wa kisheria kwa kila kata ni uwazi kuwa jamii itaelimishwa juu ya sheria mbali mbali na hata kuwezesha changamoto za mimba za utotoni na wajane kunyanyasika kwa kutojua haki zao kupungua zaidi.
"Nawaombeni sana washiriki wa mafunzo haya ambao ni madiwani na watendaji wa kata tumieni mafunzo haya kusaidia jamii kuepukana na unyanyasaji wa aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupambana na wale wanaokwamisha watoto wa kike kuendelea na masomo kwa kuwapa mimba... ila kwa LASWA naomba sana mzidi kutoa mafunzo haya kwa makatibu tafara ikiwezekana hata kwa watendaji wa vijiji ili elimu hii iwafikie watu wengi zaidi"
Kuhusu wasaidizi wa kisheria wa LASWA waliopo katika ofisi za watendaji ngazi ya kata alisema kuwa ni vizuri kila mmoja kufanya kazi yake kwa kusaidia jamii na kuepuka kutumika kukandamiza watu wasiojua sheria.
Kuwa iwapo wasaidizi hao watasaidia kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi wenye uhitaji upo uwezekano mkubwa wa jamii wilayani humo kujikita zaidi katika uzalishaji mali badala ya kupoteza pesa nyingi kwenda kutumia katika kesi mahakamani.
Meneja wa LASWA Oscar Lawa alisema kuwa kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na asasi yake ya LASWA Iringa kwa ufadhili wa LSF ya jijini Dar es salaam kwa chini ya ubalozi wa Denmark kuwa sifa ya msaidizi wa kisheria ni kuwa na akili timamu pia sifa ya kuheshimu na kulinda sheria za mbali mbali za nchi na haki za binadamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: